Thursday, December 8, 2016

1.Mwokozi Umeokoa

Mwokozi umeokoa,
Nimekuwa wako wewe.
Damu imenisafisha;
Sifa kwa mwana Kondoo.

Utukufu, Aleluya!
Sifa kwa Mwana Kondoo!
Damu imenisafisha,
Utukufu kwa Yesu!

Nilijitahidi sana
Ila sikupata raha;
Bali kwa kumtegemea
Nilipata Baraka.

Daima namwegemea
Damu ikifanya kazi,
Nikioga kwa chemichemi
Itokayo Mwokozi.

Sasa nimewekwa wakfu;
Nitaishi kwako wewe:
Fahari nashuhudia
Ya wokovu wa bure.

Nasimama kwake Yesu,
Ameponya roho yangu;
Ameniondoa dhambi,
Anifanye mzima.

Nilikuwa kifungoni,
Niliteswa na dhambi,
Nilifungwa minyororo
Yesu akanifungua.

Sifa, ameninunua!
Sifa, nguvu za wokovu!
Sifa, Bwana huhifadhi!
Sifa zake milele.

2.Twamsifu Mungu

Twamsifu Mungu kwa Mwana wa Pendo,
Aliyetufia na kupaa juu.

Aleluya! Usifiwe; Aleluya! Amin.
Aleluya! Usifiwe, utubariki.

Twamsifu Mungu kwa Roho Mtukufu,
Ametufunulia Mwokozi wetu.

Twamsifu Mwana, aliyetufia,
Aliyetwaa dhambi akazifuta.

Twamsifu Mungu wa neema yote,
Ametukomboa akatuongoza.

Tuamshe tena, tujazena pendo,
Na moyoni uwashe moto wa Roho.

3.Hata Ndimi Elfu

Hata ndimi elfu elfu,
Hazitoshi kweli
Bwana Yesu kumsifu,
Kwa zake fadhili.

Yesu, jina liwezalo
Kufukuza hofu;
Lanifurahisha hilo,
Lanipa wokovu.

Jina hilo ni uzima;
Ni afya amani;
Laleta habari njema;
Twalipiwa deni.

Yesu huvunja mapingu
Ya dhambi moyoni;
Msamaha, tena nguvu,
Twapata rohoni.

Kwa sauti yake vile
Wafu hufufuka
Wakafurahi milele,
Pasipo mashaka.

Ewe Yesu wangu Bwana,
Uwezo nipewe,
Kuhubiri kote sana,
Wote wakujue.

4.Jina La Yesu Salamu!

Jina la Yesu, Salamu!
Lisujudieni,
Ninyi Mbinguni, hukumu
Na enzi mpeni.

Enzi na apewe kwetu,
Watetea dini;
Mkuzeni Bwana wenu,
Na enzi mpeni.

Enyi mbegu ya rehema,
Nanyi msifuni;
Mmeponywa kwa neema,
Na enzi mpeni.

Wenye dhambi kumbukeni
Ya msalabani,
Kwa furaha msifuni,
Na enzi mpeni.

Kila mtu duniani
Msujudieni,
Kote-kote msifuni,
Na enzi mpeni.

Sisi na wao pamoja
Tu mumo sifani,
Milele sifa ni moja,
Ni “Enzi mpeni.”

5.Jina lake Yesu tamu


Jina lake Yesu tamu;
Tukilisikia
Hutupoza, tena hamu
Hutuondolea.

Roho iliyoumia
Kwalo hutibika,
Chakula, njaani pia;
Raha, tukichoka.

Jina hili ni msingi,
Ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili napata wingi,
Kwangu ni akiba.

Yesu, Mchunga, Rafiki
Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki,
Uzima kifoni.

Moyo wangu hauwezi,
Kukusifu kweli,
Ila sifa zangu hizi,
Bwana zikubali.

Na utakaponiita,
Kuja kwako Bwana,
Huko kwako sitaacha
Kukusifu sana.

6.Baba, Mwana, Roho


Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi,
Kila tukiamka tunakuabudu
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi,
Ewe Utatu, tunakusifu.

Baba, Mwana, Roho, wakuaminio
Wanakutolea shukrani zao
Wanakusujudia malaika nao:
Wewe u mwanzo, nawe u mwisho.

Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani,
Utukufu wako hatuoni kosa;
U Mtakatifu, nawe u mapenzi,
U peke yako, mwenzio huna.

Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi,
Ulivyoviumba vyote vyakusifu:
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi
Ewe Utatu, tunakusifu.

7.Ni Tabibu Wa Karibu


Ni tabibu wa karibu;
Tabibu wa ajabu;
Na rehema za daima;
Ni dawa yake njema.

Imbeni, malaika,
Sifa za Yesu Bwana;
Pweke limetukuka
Jina lake Yesu.

Hatufai kuwa hai,
Wala hatutumai,
Ila kweli yeye ndiye
Atupumzishaye.

Dhambi pia na hatia
Ametuchukulia;
Twendeni na amani
Hata kwake Mbinguni.

Huliona tamu jina
La Yesu Kristo Bwana,
Yuna sifa mwenye kufa
Asishindwe na kufa.

Kila mume asimame,
Sifa zake zivume;
Wanawake na washike
Kusifu jina lake.

Na vijana wote tena,
Wapendao sana
Waje kwake wawe wake
Kwa utumishi wake.