Thursday, December 8, 2016

17.Namwadama Bwana


Namwadama Bwana kwa alilonena
Njia yangu huning’azia;
Nikimridhisha atanidumisha
Taamini nitii pia.

Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii.

Giza sina kwangu wala hata wingu
Yeye mara huviondoa
Woga, wasiwasi, sononeko, basi;
Huamini nitii pia.

Masumbuko yote, sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipia;
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki
Taamini nitii pia.

Mimi sitajua raha sawasawa
Ila yote Yesu kumpa;
Napata fadhili na radhi kamili,
Taamini nitii pia.

Nitamfurahia na kumtumaini,
Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda, nikitumwa hwenda,
Huamini nitii pia.

No comments:

Post a Comment