Yesu nakupenda, U mali yangu,
Anasa za dhambi sitaki kwangu;
Na Mwokozi aliyeniokoa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
Moyo umejaa mapenzi tele
Kwa vile ulivyonipenda mbele,
Uhai wako ukanitolea
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
Ulipoangikwa Msalabani
Tusamehewe tulio dhambini;
Taji ya miiba uliyoivaa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
Niwapo hai, niwapo maiti,
Kupendana nawe kamwe siachi;
Hari za kifo zikinienea,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
Mawanda mazuri, na masikani
Niyatazamapo huko Mbinguni,
Tasema na taji nitakayovaa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
No comments:
Post a Comment