Tuesday, December 6, 2016

112.Nilikupa Wewe, Maisha Yangu


Nilikupa wewe
Damu ya moyoni,
Ili wokolewe,
Winuke ufuni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

Nilikupa miaka
Yangu duniani
Upate inuka,
Kuishi Mbinguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini:

Niliacha nuru
Za Baba, Mbinguni,
Kwingia taabu
Za ulimwenguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

Niliteswa sana,
Mateso kifoni,
Usije yaona
Hayo ya motoni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

Nimekuletea
Huku duniani
Upendo na afya
Zatoka Mbinguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

Nipe siku zako,
Udumu mwangani;
Na taabu yako,
Wingie rahani
Nafsi, pendo, mali,
Twae Imanweli.

No comments:

Post a Comment