Thursday, December 8, 2016

1.Mwokozi Umeokoa

Mwokozi umeokoa,
Nimekuwa wako wewe.
Damu imenisafisha;
Sifa kwa mwana Kondoo.

Utukufu, Aleluya!
Sifa kwa Mwana Kondoo!
Damu imenisafisha,
Utukufu kwa Yesu!

Nilijitahidi sana
Ila sikupata raha;
Bali kwa kumtegemea
Nilipata Baraka.

Daima namwegemea
Damu ikifanya kazi,
Nikioga kwa chemichemi
Itokayo Mwokozi.

Sasa nimewekwa wakfu;
Nitaishi kwako wewe:
Fahari nashuhudia
Ya wokovu wa bure.

Nasimama kwake Yesu,
Ameponya roho yangu;
Ameniondoa dhambi,
Anifanye mzima.

Nilikuwa kifungoni,
Niliteswa na dhambi,
Nilifungwa minyororo
Yesu akanifungua.

Sifa, ameninunua!
Sifa, nguvu za wokovu!
Sifa, Bwana huhifadhi!
Sifa zake milele.

2.Twamsifu Mungu

Twamsifu Mungu kwa Mwana wa Pendo,
Aliyetufia na kupaa juu.

Aleluya! Usifiwe; Aleluya! Amin.
Aleluya! Usifiwe, utubariki.

Twamsifu Mungu kwa Roho Mtukufu,
Ametufunulia Mwokozi wetu.

Twamsifu Mwana, aliyetufia,
Aliyetwaa dhambi akazifuta.

Twamsifu Mungu wa neema yote,
Ametukomboa akatuongoza.

Tuamshe tena, tujazena pendo,
Na moyoni uwashe moto wa Roho.

3.Hata Ndimi Elfu

Hata ndimi elfu elfu,
Hazitoshi kweli
Bwana Yesu kumsifu,
Kwa zake fadhili.

Yesu, jina liwezalo
Kufukuza hofu;
Lanifurahisha hilo,
Lanipa wokovu.

Jina hilo ni uzima;
Ni afya amani;
Laleta habari njema;
Twalipiwa deni.

Yesu huvunja mapingu
Ya dhambi moyoni;
Msamaha, tena nguvu,
Twapata rohoni.

Kwa sauti yake vile
Wafu hufufuka
Wakafurahi milele,
Pasipo mashaka.

Ewe Yesu wangu Bwana,
Uwezo nipewe,
Kuhubiri kote sana,
Wote wakujue.

4.Jina La Yesu Salamu!

Jina la Yesu, Salamu!
Lisujudieni,
Ninyi Mbinguni, hukumu
Na enzi mpeni.

Enzi na apewe kwetu,
Watetea dini;
Mkuzeni Bwana wenu,
Na enzi mpeni.

Enyi mbegu ya rehema,
Nanyi msifuni;
Mmeponywa kwa neema,
Na enzi mpeni.

Wenye dhambi kumbukeni
Ya msalabani,
Kwa furaha msifuni,
Na enzi mpeni.

Kila mtu duniani
Msujudieni,
Kote-kote msifuni,
Na enzi mpeni.

Sisi na wao pamoja
Tu mumo sifani,
Milele sifa ni moja,
Ni “Enzi mpeni.”

5.Jina lake Yesu tamu


Jina lake Yesu tamu;
Tukilisikia
Hutupoza, tena hamu
Hutuondolea.

Roho iliyoumia
Kwalo hutibika,
Chakula, njaani pia;
Raha, tukichoka.

Jina hili ni msingi,
Ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili napata wingi,
Kwangu ni akiba.

Yesu, Mchunga, Rafiki
Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki,
Uzima kifoni.

Moyo wangu hauwezi,
Kukusifu kweli,
Ila sifa zangu hizi,
Bwana zikubali.

Na utakaponiita,
Kuja kwako Bwana,
Huko kwako sitaacha
Kukusifu sana.

6.Baba, Mwana, Roho


Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi,
Kila tukiamka tunakuabudu
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi,
Ewe Utatu, tunakusifu.

Baba, Mwana, Roho, wakuaminio
Wanakutolea shukrani zao
Wanakusujudia malaika nao:
Wewe u mwanzo, nawe u mwisho.

Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani,
Utukufu wako hatuoni kosa;
U Mtakatifu, nawe u mapenzi,
U peke yako, mwenzio huna.

Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi,
Ulivyoviumba vyote vyakusifu:
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi
Ewe Utatu, tunakusifu.

7.Ni Tabibu Wa Karibu


Ni tabibu wa karibu;
Tabibu wa ajabu;
Na rehema za daima;
Ni dawa yake njema.

Imbeni, malaika,
Sifa za Yesu Bwana;
Pweke limetukuka
Jina lake Yesu.

Hatufai kuwa hai,
Wala hatutumai,
Ila kweli yeye ndiye
Atupumzishaye.

Dhambi pia na hatia
Ametuchukulia;
Twendeni na amani
Hata kwake Mbinguni.

Huliona tamu jina
La Yesu Kristo Bwana,
Yuna sifa mwenye kufa
Asishindwe na kufa.

Kila mume asimame,
Sifa zake zivume;
Wanawake na washike
Kusifu jina lake.

Na vijana wote tena,
Wapendao sana
Waje kwake wawe wake
Kwa utumishi wake.


8.Taji mvikeni


Taji mvikeni,
Taji nyingi tena,
Kondoo mwake kitini,
Bwana wa mabwana;
Name tamsifu
Alikufa kwangu,
Ni mfalme mtukufu,
Mkuu wa Mbingu.

Taji mvikeni
Mwana wa bikira;
Anazovaa kichwani
Aliteka nyara;
Shiloh wa wanabii,
Mchunga wa watu,
Shina na tanzu vya Yese,
Wa Bethirehemu.

Taji mvikeni
Bwana wa mapenzi;
Jeraha zake ni shani
Ni vito vya enzi,
Mbinguni hakuna
Hata malaika
Awezaye kuziona
Pasipo kushangaa.

9.Yesu kwetu ni rafiki


Yesu kwetu ni rafiki,
Hwamiwa haja pia;
Tukiomba kwa Babaye
Maombi asikia;
Lakini twajikosesha,
Twajitweka vibaya;
Kwamba tulimwomba Mungu
Dua angesikia.

Una dhiki na maonjo?
Una mashaka pia.
Haifai kufa moyo,
Dua atasikia
Hakuna mwingine mwema
Wa kutuhurumia;
Atujua tu dhaifu;
Maombi asikia.

Je, hunayo hata nguvu,
Huwezi kuendelea,
Ujapodharauliwa
Ujaporushwa pia,
Watu wange kudharau,
Wapendao dunia,
Hukwambata mikononi,
Dua atasikia.

10.Usinipite!


Usinipite Mwokozi,
Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite.

Yesu,Yesu,
Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite.

Kiti chako cha rehema,
Nakitazama;
Magoti napiga pale,
Nisamehewe.

Sina ya kutegemea,
Ila Wewe tu;
Uso wako uwe kwangu;
Nakuabudu.

U Mfariji peke yako;
Sina Mbinguni,
Wala duniani pote,
Bwana mwingine.

11.Nina haja nawe


Nina haja nawe
Kila saa;
Hawezi mwingine
Kunifaa.

Yesu, nakuhitaji
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi,
Nakujia.

Nina haja nawe;
Kaa nami,
Na maonjo haya,
Hayaumi.

Nina haja nawe;
Kila hali,
Maisha ni bure,
Uli mbali.

Nina haja nawe,
Nifundishe
Na ahadi zako
Zifikishe.

Nina haja nawe,
Mweza yote,
Ni wako kabisa
Siku zote.

13.Tafuta daima utakatifu


Tafuta daima utakatifu;
Fanya urafiki na Wakristo tu;
Nena siku zotena Bwana wako,
Baraka uombe kwa kila jambo.

Tafuta daima utakatifu;
Uwe peke yako ukimwabudu;
Ukimwangalia mwokozi wako,
Utabadilishwa kama alivyo.

Tafuta daima utakatifu;
Kiongozi wako aew Yesu tu;
Katika furaha au huzuni
Dumu kumfuata Yesu Mwokozi.

Tafuta daima utakatifu;
Umtawaze Roho moyoni mwako;
Akikuongoza katika haki,
Hufanywa tayari kwa kazi yake.

12.Ewe Roho wa Mbinguni


Ewe Roho wa Mbinguni
Uje kwetu sasa.
Ufanye makazi yako
Ndani ya Kanisa.

Ndiwe mwanga, umulike
Tupate jikana;
Mengi kwetu yapunguka,
Tujalize, Bwana.

Ndiwe Moto, teketeza
Taka zetu zote:
Moyo na iwe sadaka
Ya Mwokozi, yote.

Ndiwe Umande, na kwako
Tutaburudika,
Nchi kavu itakuwa
Ni yenye Baraka.

Roho wa Mbinguni uwe
Nasi hapa chini,
Mwili uufananishe
Na kichwa Mbinguni.

14.Yesu kwa imani


Yesu kwa imani,
Nakutumaini,
Peke yako;
Nisikie sasa,
Na kunitakasa,
Ni wako kabisa
Tangu leo.

Nipe nguvu pia
Za kusaidia
Moyo wangu;
Ulikufa wewe,
Wokovu nipewe
Nakupenda wewe,
Bwana wangu.

Hapa nazunguka
Katika mashaka,
Na matata;
Palipo na giza
Utaniongoza
Hivi nitaweza
Kufuata.

Takuwa mzima
Nivushe salama
Mautini;
Sina hofu kamwe
Ukiwapo name
Nami nikwandame
Siku zote.

16.Kumtegemea Mwokozi


Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa;
Kukubali neno lake
Nina raha moyoni.

Yesu,Yesu namwamini,
Nimemwona thabiti;
Yesu,Yesu,yu thamani,
Ahadi zake kweli.

Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa,
Kuamini damu yake
Nimeoshwa kamili.

Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa,
Kwake daima napata
Uzima na amani.

Nafurahi kwa sababu
Nimekutegemea;
Yesu,Mpendwa na Rafiki
Uwe nami dawamu.

15.Chakutumaini Sina


Ila damu yake Bwana,
Sina wema wa kutosha
Dhambi zangu kuziosha;

Kwake Yesu nasimma,
Ndiye mwamba: ni salama
Ndiye mwamba: ni salama.

Njia yangu iwe ndefu
Yeye hunipa wokovu;
Mawimbi yakinipiga
Nguvu zake ndiyo nanga.

Damu yake na sadaka
Nategemea daima,
Yote chini yakiisha
Mwokozi atanitosha.

Nikiitwa hukumuni,
Rohoni nina amani
Nikivikwa haki yake
Sina hofu mbele zake.

17.Namwadama Bwana


Namwadama Bwana kwa alilonena
Njia yangu huning’azia;
Nikimridhisha atanidumisha
Taamini nitii pia.

Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii.

Giza sina kwangu wala hata wingu
Yeye mara huviondoa
Woga, wasiwasi, sononeko, basi;
Huamini nitii pia.

Masumbuko yote, sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipia;
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki
Taamini nitii pia.

Mimi sitajua raha sawasawa
Ila yote Yesu kumpa;
Napata fadhili na radhi kamili,
Taamini nitii pia.

Nitamfurahia na kumtumaini,
Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda, nikitumwa hwenda,
Huamini nitii pia.

18.Akifa Yesu nikafa naye


Akifa Yesu nikafa naye
Uzima upya huishi naye;
Humtazama mpaka nje:
Nyakati zote ni wake yeye.

Nyakati zote nimo pendoni,
Nyakati zote ni uzimani,
Humtazama hata atokee,
Nyakati zote mimi ni wake.

Vita sipigi visivyo haki,
Na Bwana wangu hapiganiki;
Beramu yake haitwaliki,
Napo po pote hila sitaki.

Sina mashaka, akawa mbali;
Mizigo yote aihimili;
Ananituliza Imanweli,
Nyakati zote mimi husali.

Sina huzuni na mimi sidhii;
Simwagi chozi, wala siguni;
Sikuti afa, ila kitini
Daima hunifikiri mimi.

Kila unyonge huusikia;
Kila ugonjwa kwake hupoa;
Yesu ni mwenye kuniokoa
Nyakati zote hunijalia.


19.Ndiyo dhamana, Yesu wangu


Ndiyo dhamana, Yesu wangu;
Hunipa furaha za Mbingu;
Mrithi wa wokovu wake
Nimezawa kwa Roho yake.

Habari njema, raha yangu
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu
Yesu ndiye mwokozi wangu.

Kumsalimu moyo wangu,
Mara namwona raha yangu;
Aniletea malaika,
Wananilinda, taokoka.

Sina Kinyume, nashukuru,
Mchana kutwa huja kwangu;
Usiku kucha kuna nuru;
Mwokozi wangu; ndimi huru.

Hali na mali anitwaa!
Mara namwona anifaa,
Nami nangoja kwa subira;
Akiniita, nije mara.

20.Ninaye Rafiki naye


Ninaye Rafiki naye
Alinipenda mbele;
Kwa kamba za pendo zake
Nimefungwa milele;
Aukaza moyo wangu,
Uache mageule,
Mimi wake, yeye wangu;
Ndimi naye milele.

Ninaye rafiki ndiye
Aliyenifilia;
Alimwaga damu yake
Kwa watu wote pia;
Sina kitu mimi tena,
Nikiwa navyo tele;
Pia vyote ni amana
Ndimi wake milele.

Ninaye rafiki naye
Uwezo amepewa;
Atanilinda mwenyewe,
Juu tachukuliwa;
Nikitazama Mbinguni,
Hupata nguvu tele;
Sasa natumika chini,
Kisha juu milele.

Ninaye rafiki naye,
Anao moyo mwema;
Ni mwalimu, kiongozi,
Mlinzi wa daima;
Ni nani wa kunitenga
Na mapenzi ya mbele?
Kwake nimetia nanga,
Ndimi wake milele.

21.Roho Yangu Hima


Roho yangu hima, na taa yako
Kaiwashe vyema, hapa si pako;
Nguvu zote pia za duniani
Hazitakudhuru ukiamini.

Yesu yuko mbele, Yesu yu nyuma,
Yesu vivyo kando, walindwa vyema.

Adui shetani, na nguvu zake,
Bwana ameshinda, kwa kifo chake;
Wewe nguvu huna, huna kabisa,
Ndiwe mpungufu, mnyonge hasa.

Toka na mapema, mbele ya wote,
Omba, bisha sana, maisha yote;
Vita vikaliko, macho ukae,
Jivike silaha, nawe sishindwe.

Bwana Yesu ndiye kwako mchunga,
Neno lake Bwana ndilo upanga;
Mbingu zitakwisha, na nchi pia,
Neno lake Bwana laendelea.


22.Kale nilitembea


Kale nilitembea
Nikilemewa dhambi
Nilikosa msaada,
kuniponya mateso.

Usifiwe Msalaba!
Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote,
Asifiwe Mwokozi!

Hata nilipofika,
Mahali pa Msalaba,
Palinifaa sana,
Sitasahau kamwe.

Hicho ndicho chanzo,
Cha kufurahi kwangu.
Hapo ndipo mzigo,
Uliponituliwa.

Panapo msalaba,
Kinatolewa cheti,
Cha kuingia Mbinguni,
Kisicho cha kanisa.

Yule Bwana mjinga,
Likwenda bila cheti,
Kitumai kwingia,
Kama walio nacho.

Lipofika langoni,
Akaulizwa cheti,
Cha kumwonyesha Bwana,
Akakutwa hanacho.

Lituhuzunishalo,
Ni ninyi msio nacho,
Kuwa kama mjinga,
Kwa siku ya arusi!

Ubavuni mwa Yesu,
Mlitokea damu,
Chemchemi ya uzima,
Itakasayo roho.

Jitahidi wingie,
Damuni mwa Mwokozi,
Utafutiwa dhambi,
Toka rohoni mwako

23.Ni Salama Rohoni Mwangu


Nionapo amani kama shwari,
Ama nionapo shida;
Kwa mambo yote umenijulisha,
Ni salama rohoni mwangu.

Salama rohoni,
Ni salama rohoni mwangu.

Ingawa shetani atanitesa,
Nitajipa moyo kwani
Kristo ameona unyonge wangu,
Amekufa kwa roho yangu.

Dhambi zangu zote, wala si nusu,
Zimewekwa msalabani;
Wala sichukui laana yake,
Ni salama rohoni mwangu.

Ee Bwana himiza siku ya kuja,
Panda itakapolia;
Utakaposhuka sitaogopa
Ni salama rohoni mwangu.

24.Mwokozi Moyoni Mwangu



Tangu siku hiyo aliponijia,
Akae moyoni mwangu,
Sina giza tena, ila mwanga pia
Kwa Yesu mwokozi wangu.

Amani moyoni mwangu,
kwa Yesu, Mwokozi wangu;
Sina shaka kamwe,
Kwa sababu yeye,
Yu nami moyoni mwangu.

Sina haja tena, ya kutanga-tanga,
Ndiye kiongozi wangu.
Dhambi zangu zote zimeondolewa,
Na Yesu, Mwanawe Mungu.

Matumaini yangu ni ya hakika,
Katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu zimeondoka,
kwa kuwa ninaye Yesu.

Siogopi tena, nikiitwa kufa,
Yu nami daima, Yesu.
Mlango wa Mbinguni ni yeye pia,
“Tapita humo kwa damu.”

Nitaketi na yeye huko milele,
Nisifu Mwokozi wangu.
Nina raha moyoni majira yote,
Kwa Yesu, Mwanawe Mungu.

25.Nimekombolewa na Yesu


Nimekombolewa na Yesu
Aliyenirehemia;
Kwa bei ya mauti yake
Nimekuwa mtoto wake.

Kombolewa!
Nakombolewa na damu;
Kombolewa!
Mimi mwana wake kweli.

Kukombolewa nafurahi,
Kupita lugha kutamka;
Kulionyesha pendo lake,
Nimekuwa mtoto wake.

Nitamwona uzuri wake,
Mfalme wangu wa ajabu;
Na sasa najifurahisha,
Katika neema yake.

Najua taji imewekwa
Mbinguni tayari kwangu;
Muda kitambo atakuja,
Ili alipo, niwepo.

26.Yesu Unipendae


Yesu unipendaye
Kwako nakimbilia,
Ni wewe utoshaye,
Mwovu akinijia;
Yafiche ubavuni,
Mwako maisha yangu;
Nifiikishe mbinguni
Wokoe moyo wangu.

Ngome nyingine sina;
Nategemea kwako.
Usinitupe Bwana ,
Nipe neema yako,
Ninakuamania
Mwenye kuniwezesha;
Shari wanikingia,
Vitani wanitosha.

Nakutaka Mpaji
Vyote napata kwako;
Niwapo muhitaji,
Utanijazi vyako;
Nao waangukao
Wanyonge wape nguvu;
Poza wauguao,

Uongoze vipofu.
Bwana umeniosha
Moyo kwa damu yako;
Neema ya kutosha
Yapatikana kwako;
Kwako Bwana naona
Kisima cha uzima;
Mwangu moyoni Bwana,
Bubujika daima.

27.Mungu Ni Pendo


Mungu ni pendo, apenda watu;
Mungu ni pendo, anipenda

Sikilizeni furaha yangu,
Mungu ni pendo, anipenda.

Nilipotea katika dhambi,
Nikawa mtumwa wa shetani.

Akaja Yesu kuniokoa,
Yeye kanipa kuwa huru

Sababu hii namtumikia,
Namsifu yeye siku zote.

28.Anipenda ni kweli


Anipenda ni kweli;
Mungu anena hili;
Sisi wake watoto;
kutulinda si zito.

Yesu anipenda,
Yesu anipenda,
Kweli anipenda,
Mungu amesema.

Kwa kupenda akafa
Niokoke na kufa;
Atazidi taka,
Sana ataniweka.

Anipenda kabisa;
Niuguapo sasa
Anitunza Mbinguni
Nniliyelala chini.

Kunipenda haachi,
Tu sote hapa chini
Baada ya mashaka
Kwake tanipeleka.

29.Baba yetu aliye Mbinguni


Baba yetu aliye Mbinguni
Amenifurahisha yakini
Kuniambia mwake chuoni
Ya kuwa nami Yesu pendoni.

Anipenda Mwokozi Yesu,
Anipenda, anipenda;
Anipenda Mwokozi Yesu,
Anipenda mimi.

Nimuachapo kutanga mbali,
Yeye yu vivyo, hupenda kweli,
Hunirejeza kwake moyoni;
Kweli yu nami Yesu pendoni.

Anipenda! Nami nampenda;
Kwa wokovu alionitenda;
Akanifia Msalabani
Kwa kuwa nami Yesu pendoni.

Haya kujua yanipa raha;
Kumuamini kuna furaha;
Humfukuza mara shetani,
Kwona yu nami Yesu Pendoni.

Sifa ni nyingi asifiwazo,
Moja ni sana katika hizo,
Wala siachi, hata Mbinguni,
Kwimba, “Yu nami Yesu pendoni”.

30.Nilikuwa kondoo aliyepotea


Nilikuwa kondoo aliyepotea,
Sikupenda zizi kamwe, ila kutembea
Nilikuwa mwana asiyesikia,
Sikupenda baba yangu wala kutulia.

Na mchunga mwema alinitafuta,
Baba kwa mapenzi ndiye aliyenivuta;
Karibu ya kufa, kwa kiu na kwa njaa,
Waliniona mnyonge, waliniokoa.

Yesu ni mchunga, mwenziwe hapana,
Aliosha taka zangu, dhambi nyingi sana;
Kwa vidonda vyangu alitia dawa.
Ndiye aliyenipata, na kwake nalindwa.

Nilikuwa kondoo aliyepotea
Sasa nampenda Baba, na mchunga pia;
Kwanza nilitanga na kukosa sana,
Hivi nyumbani mwa Baba sipotei tena.

31.Msingi Imara


Msingi imara, enyi wa kweli,
Umekwisha pigwa kwa neno hili;
Aongeze lipi? Mnayo pia
Kwa Yesu mliomkimbilia.

Wambiwapo vuka maji ya giza,
Mito ya mashaka taipunguza;
Takupa nawe, nikuwezeshe,
Ipata kufaa, isikutishe!

Utakapopishwa ndani ya moto
Nnguvu nitakupa, upate pato;
Huteketezwi, ila taka zako,
Na zitasalia dhahabu zako.

Hata zije mvi, walio wangu
Hawaoni kwisha mapenzi yangu;
Nazo zitakapowenea, ndipo
Mabegani mwangu niwatwekapo.

Na mtu aliyenitegemea
Kamwe kwa adui sitamtia;
Nguvu za jehanam zijapotisha,
Mtu wangu kamwe sitamuacha.

32.Yesu Awakubali


Wakosa
Yesu awakubali,
Wakosa, wahalifu,
Wambieni wa mbali
Habari ya wokovu.

Tangazeni kwa bidii,
“Akubali wakosa!”
Liwe neno dhahiri,
“Akubali wakosa!”

Awakubali Bwana
Neno lake amini
Watu kila aina
Waje kwake tengoni.

Mimi ni safi moyo
Na mbele ya sharia,
Aliye safi roho
Kwake ilitimia.

Akubali wakosa;
Nami anikubali;
Alivyonitakasa
Mbinguni niwasili.


33.Dhambi Ikikulemea


Dhambi ikikulemea,
Kwa Bwana rehema;
Hivi sasa tegemea
Neno la salama.

Tegemea, tegemea,
akwita sasa.
Ni Mwokozi, ni
Mwokozi; amini sasa.

Yesu amemwaga damu
Ya nyingi baraka;
Nawe sasa oga mumu
Zioshwamo taka.

Ni njia yeye hakika
Hwongoza rahani;
Usikawe kumshika,
Uwe barakani.

Karibu nawe wingie
Mwetu safarini,
Twende tukamwamkie,
Milele Mbinguni.

34.Njoni Wenye Dhambi


Njoni! Njoni! Wenye dhambi,
Njoni, msikawie;
Yesu awangojea ndiye awapendaye;
Ajuaye awezaye
kuwaponya ni Yeye.

Ewe muhitaji uje;
Anakukaribisha,
Imani, kweli, na toba,
Neema ya kutosha,
Jua sana, kwake Bwana
Bure utapata.

Njoni, mliolemewa
Na dhambi ya Adamu;
Mkingoja kujiponya
Mtapotea mumu;
Si wa haki, ni wakosa
Waoshwao kwa damu.

Ikamtokea dhiki,
Mle Gethisemani;
Kisha alipoangikwa
Akalia mtini;
” Imekwisha”, alitosha
Dhabihu ya thamani.

Kristo aliye Mbinguni
Hutuombea huko;
Basi mtumai yeye;
Kamwe mwingine hako
Yesu pweke, Yesu pweke,
Ndiye Mwokozi wako.

Wamsifu-sifu sana
Mbinguni malaika;
Wachanganya nyimbo zao
Na waliookoka:
Aleluya wataimba
Waliooshwa taka.

35.Twende kwake


Twende kwake, twende kwake, kwake Yesu sasa,
Sasa twende kwake, kwake Yesu sasa!

Akwokoe. akwokoe, Bwana Yesu sasa!
Sasa akwokoe, Bwana Yesu, sasa!

Msadiki, msadiki, Bwana Yesu sasa,
Sasa msadiki, Bwana Yesu sasa!

Anaweza, anaweza, Bwana Yesu sasa,
Sasa anaweza, Bwana Yesu sasa!

Anapenda, anapenda, Bwana Yesu, sasa,
Sasa anapenda, Bwana Yesu sasa!
Njoo hima, njoo hima, kwake Yesu sasa,
Sasa njoo hima, kwake Yesu, sasa!

36.Anisikiaye, Aliye Yote


Anisikiaye, aliye yote;
Sasa litangae, wajue wote,
Duniani kote neno wapate,
Atakaye na aje!

Ni “Atakaye”, ni “atakaye”,
Pwani hata bara, na litangae;
Ni Baba Mpenzi alinganaye
Atakaye na aje.

Anijiliaye, Yesu asema,
Asikawe, aje hima mapema;
Ndimi njia, kweli, ndimi uzima;
Atakaye na aje!

Atakaye aje, ndivyo ahadi;
Atakaye hiyo, haitarudi!
Atakaye lake, ni la abadi!
Atakaye na aje.

37.Waitwa, Mwovu, na Bwana


Waitwa, mwovu, na Bwana
Umwendee hima sana,
Usafiwe dhambi zako,
Humwoni ni mwema kwako?

Unaitwa! Itika tu!
Umwendee Bwana Yesu!
Sifiche makosa yako,
Uungame dhambi zako!
Kristo tu umuamini,
Ndiyo njia ua Mbinguni.

Alilipa damu yake
Ili kukukweza kwake;
Alikufa yeye Bwana,
Mimi nawe tuwe wema.

Ukifanywa kuwa mwema
Mwishoni utasimama,
Utaingia rahani
Na wapenzi wa zamani.

Ni mwanga tu, nchi ile;
Uovu hauko kule,
Kwamba wataka ufike
Sharti huku uosheke.

38.Twende Kwa Yesu


Twende kwa Yesu mimi nawe,
Njia atwonya tuijue
Imo Chuoni; na Mwenyewe,
Hapa asema, Njoo!

Na furaha tutaiona,
Mioyo ikitakata sana,
Kwako, Mwokozi, kuonana,
Na milele kukaa.

”Wana na waje”, atwambia,
Furahini mkisikia,
Ndiye mfalme wetu pia,
Na tumtii, Njoo.

Wangojeani? Leo yupo;
Sikiza sana asemapo;
Huruma zake zikiwapo,
Ewe kijana, Njoo.

39.Mwenye Dhambi Huna Raha


Mwenye dhambi huna raha,
Sikiza nakusihi,
Utapata msamaha
Kwake Yesu Mwokozi!
Njoo hima, njoo hima,
Naye atafurahi.

Yesu anakwita sana
Naye yuko Mbinguni;
Hofu ya kifo hapana
Kwake ukiamini.
Njoo hima, njoo hima,
Utapata amani.

Hatakwita siku zote;
Ni ya sasa nafasi.
Lete na uchafu wote,
Kukawa haipasi.
Njoo hima, njoo hima,
Ni wokovu halisi.

Uzima uko kwa Bwana
Twae uzima hasa
Bure unapatikana,
Wokovu twae sasa!
Njoo hima, njoo hima,
Twae utakatifu.

40.Nasikia Kwitwa


Nasikia kwitwa
Na sauti yako
Nikasafiwe kwa damu
Ya kwangikwa kwako.

Nimesogea Mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.

Ni mnuonge kweli,
Umenipa nguvu,
Ulivyonisafi taka,
Ni utimilivu.

Yesu hunijuvya;
Mapenzi, imani;
Tumai, amani, radhi,
Hapa na Mbinguni.

Huipa imara,
Kazi yake, ndani:
Huongezeka neema,
Ashindwe Shetani.

Huishuhudia,
Myoyo ya imani
Ya kuzipata ahadi,
Wakimuamini.

Napata wokovu,
Wema na neema;
kwako Bwana nina nguvu
Na haki daima.

41. Yesu Aliniita


Yesu aliniita, “njoo,
Raha iko kwangu,
Kichwa chako ukilaze
Kifuani mwangu.”

Nilikwenda kwake mara,
Sana nilichoka;
Nikapata kwake raha,
Na furaha tena.

Yesu aliniita, “njoo,
Kwangu kuna maji,
Maji ya uzima, bure,
Unywe uwe hai, ”

Nilikwenda kwake mara
Na maji nikanywa:
Naishi kwake, na kiu
Kamwe sina tena.

Yesu aliniita, “njoo,
Dunia ni giza,
Ukinitazama nuru
Takung’arizia.”

Nilikwenda kwake mara
Yeye jua langu,
Ni kila wakati mwanga
Safarini mwangu.

42.Kivulini Mwa Yesu


Kivulini mwa Yesu kuna Kituo:
Kituo mbali na hamu, kituo kilicho tamu.

Kivulini mwa Yesu kuna kituo;
kivulini mwa Yesu kuna kituo;
Raha tu, mle; amani tupu,
Furaha tele; kivulini mwa Yesu
Raha tu, mle; amani tupu,
Furaha tele; kivulini mwa Yesu.

Kivulini mwa Yesu nina amani
Iliyopita fahamu, tena itakayodumu.

Kivulini mwa Yesu, nina furaha;
Furaha yenye fahari, ya kueneza habari.

43.Yesu Akwita


Yesu akwita, chanena Chuo:
Uje leo, uje leo;
Kwani kusita? Akwita, Njoo;
Unatanga upeo.

Hwita leo, hwita leo.
Yesu akwita kwa upole akwita leo.

Waliochoka, wapumzike,
Hwita leo, hwita leo:
Wenye mizigo, wakamtweke,
wapate mapumuo.

Anakungoja, uliye yote,
Uje leo, uje leo;
Uliyekosa usijifiche:
Woshwe, uvikwe nguo.

Yesu asihi wakawiao,
Waje leo, waje leo.
Watafurahi waaminio;
Usije kwani? Njoo.

44.Kukawa Na Giza Dunia Yote


Kukawa na giza dunia yote,
Ni Mwanga wa ulimwengu,
Ikaisha ulipokuja yote,
Ni mwanga wa ulimwengu.

Jua, Yesu hana mwenziwe!
Nalipofuka kama wewe:
Nakuombea umwone nawe,
Ni mwanga wa ulimwengu.

Hatuna giza tudumuo mwake,
Ni mwanga wa ulimwengu;
Tumwandamiapo nyayoni mwake
Ni mwanga wa ulimwengu.

Enyi wa gizani wenye kutanga!
Ni mwanga wa ulimwengu,
Kaulekeeni, mpate lenga;
Ni mwanga wa ulimwengu.

Tutamwona Mwokozi juu ya mbingu
Ni mwanga wa ulimwengu:
Ni nuru za mbingu kondoo wa Mungu
Ni mwanga wa ulimwengu.

45.Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu


Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu
Hivi sasa upate ishi.
Mwenye – dhambi dhaifu, mtazame tu
Wala usifanye tashwishi.

Tazama! Tazama! Tazama uishi!
Mtazame huyo aliyeangikwa juu
Hivi sasa upate ishi.

Kama mwana kondoo hakuondoa dhambi,
Na makosa yako maovu!
Kama deni zetu zote hakulipa
Mbona imemwagika damu?

Si kutubu na sala ikomboayo,
Ila damu ndiyo salama;
Na aliyeimwaga aweza, sasa,
Dhambi zako kukufutia.

Usiwe na shaka, Mungu amesema,
Hakuna alilolisaza;
Hapo alipokuja alitimiza
Kazi zote alizoanza.

Basi twae uzima, kwa kufurahi
Upokee kwa Bwana, sasa;
Ujijue hakika kwake kuishi
Yesu aishiye kabisa.

46.Twae Wangu Uzima


Twae wangu uzima,
Sadaka ya daima;
Twae saa na siku,
Zikutukuze huku.

Twae mikono nayo
Ifanye upendavyo,
Twae yangu miguu
Kwa wongozi wako tu.

Twae sauti yangu,
Niimbe kwa Mungu tu;
Itwae na midomo,
Ijae neno lako.

Twae dhanabu pia,
Na yote ya dunia;
Twae yangu hekima,
Upendavyo tumia.

Nia itwae, Mungu,
Haitakuwa yangu;
Twae moyo; ni wako,
Uwe makazi yako.

Twae mapenzi yangu,
Sifa za moyo wangu;
Twae kabisa nafsi
Nniwe wako halisi.

48.Naweka Dhambi Zangu


Naweka dhambi zangu
Juu yake Bwana
Kuziondoa, kwangu
Hulemea sana;
Na uaili wangu
Ameuondoa;
Dawa yangu ni damu,

Kwa hiyo napoa.
Na uhitaji wangu
Nitamjuvisha
Kwa upungufu wangu
Yeye anatosha;
Majonzi yangu yote
Na mizigo yangu,
Atachukua vyote

Yesu Bwana wangu.
Na roho yangu nayo,
Imechoka sana;
Namletea hiyo
Ilindwe na Bwana;
Ni jema jina lake,
Nalo lapendeza,
Imanweli na kwake

tutalitukuza.
Natamani daima
Niwe kama Bwana,
Mpole, tena mwema,
Wa mapenzi sana;
Zaidi natamani
Kwenda kwake juu,
Nikaone mbinguni
Enzi yake kuu.

47.Ni WaKo Wewe


Ni wako wewe, nimekujua,
Na umeniambia;
Lakini Bwana, nataka kwako nizidi kusongea.

Bwana vuta, vuta, nije nisongee,
Sana, kwako mtini.
Bwana vuta, vuta, nije nisongee,
Pia damu ya thamani.

Niweke sasa nikatumike
Kwa nguvu za neema;
Uyapendayo nami nipende,
Nizidi kukwandama.

Nina furaha tele kila saa
Nizungumzavyo kwako,
Nikuombapo nami napata kujua nia yako.

Mapenzi yako hayapimiki,
Ila ng’ambo ya liko.
Anasa pia sitazijua,
Bila kufika kwako.

49.Nitwae Hivi Nilivyo


Nitwae hivi nilivyo,
Umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita,
Bwana Yesu,naja,naja.

Hivi nilivyo;si langu
Kujiosha roho yangu;
Nisamehe dhambi zangu,
Bwana Yesu,naja,naja.

Hivi nilivyo; sioni
Kamwe furaha moyoni;
Daima ni mashakani,
Bwana Yesu,naja,naja.

Hivi nilivyo kipofu,
maskini na mpungufu;
Wewe u mtimilifu;
Bwana Yesu,naja,naja.

Nawe hivi utanitwaa;
Nisithubutu kukawa,
Na wewe hutanikataa,
Bwana Yesu,naja,naja.

Hivi nilivyo;mapenzi
Yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi,
Bwana Yesu,naja,naja.

51.Mungu Twatoa Shukrani


Bwana Yesu atakuja, Vumilia!
Omba, ukiwa na haja, Vumilia!
Mbingunu Mungu aliko, Mwamini Mwokozi wako,
Nawe utafika huko, Vumilia!

Ikikucheka dunia, Vumilia!
Mwovu atakuvizia, Vumilia!
Hataweza kukushinda, Bwana Yesu akulinda,
Roho yako, akupenda, Vumilia!

Na ukiwa hatarini, Vumilia!
Dhiki nyingi duniani, Vumilia!
Vyatupasa kuyakuta, Majaribu na matata,
Na Bwana hakutuficha; Vumilia!

Adui wakikutana, Vumilia!
Na ndugu wakikukana, Vumilia!
Zote, zote zitakwisha, Nguvu zote za kutisha
Mungu chini atashusha; Vumilia!

Moyoni una majonzi, Vumilia!
Ndiyo bonde-ya-machozi, Vumilia!
Hima tutaandamana, Kwetu Mbinguni na Bwana
Tena hatutaachana; Vumilia!

50.Yesu Nakupenda, U Mali Yangu


Yesu nakupenda, U mali yangu,
Anasa za dhambi sitaki kwangu;
Na Mwokozi aliyeniokoa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

Moyo umejaa mapenzi tele
Kwa vile ulivyonipenda mbele,
Uhai wako ukanitolea
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

Ulipoangikwa Msalabani
Tusamehewe tulio dhambini;
Taji ya miiba uliyoivaa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

Niwapo hai, niwapo maiti,
Kupendana nawe kamwe siachi;
Hari za kifo zikinienea,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

Mawanda mazuri, na masikani
Niyatazamapo huko Mbinguni,
Tasema na taji nitakayovaa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

53.Wewe Umechoka Sana?


Wewe umechoka sana?
Wataka raha?
Kwake Yesu utapata furaha.

Alama anazo yeye?
Sasa! makovu ya mikono, na miguu,
Na mbavu.

Nacho kimivukwa taji
Kichwa cha huba?
Alivikwa taji kweli miiba.

Huku nikimfuata nipate nini?
Maonjo nje na ndani amani.
Kwamba namwandama Bwana,

Mwisho ni nini?
Ni furaha na salama
Mbinguni.

52.Yote Namtolea Yesu


Yote namtolea Yesu
Nampa moyo wote,
Nitampenda siku zote,
Namwandama kila saa.

Yote kwa Yesu,
Yote kwa Yesu,
Yote kwako, Ee mwokozi,
Natoa sasa.

Yote namtolea Yesu,
Nainamia pake;
Nimeacha na anasa,
Kwako Yesu nipokee,

Yote namtolea Yesu,
Nifanye niwe wako;
Nipe Roho yako, Bwana,
Anilinde daima,

Yote namtolea Yesu,
Nami naona sasa;
Furaha ya ukombozi,
Nasifu jina lake,

55.Nipe Moyo Wenye Sifa


Nipe moyo wenye sifa
Sio wa utumwa;
Moyo ulionyunyizwa
Damu ya thamani.

Moyo msikizi, moyo
Wa kunyenyekea,
Moyo utawaliwao
Na Mwokozi pia.

Mwenye kutubu, mnyonge,
Sadiki, amini;
Kamwe, kamwe asitengwe
Akaaye ndani.

Mpya, mwema na mawazo
Mwingi wa mapenzi
Nawe uwe kielelezo
Moyo wa Mwokozi.

Ni uule moyo wako;
Moyo wa huruma
Yesu, natamani kwako
Kukujua vyema.

Na ya midomo matunda
Yako, nipe nami;
Amani isiyokoma
Iwe yangu mimi.

Nitie yako tabia,
Inishukie juu;
Jina lako nipe pia,
Ndilo la upendo.

Ni wa baba utukufu;
Mwana atukuke;
Na roho Mtakatifu
U utatu pweke.

54.Yesu Nataka Kutakaswa Sana


Yesu nataka kutakaswa sana,
Nataka moyo uwe enzi yako.
Ukiangushe kilichoinuka
Unioshe sasa niwe mweupe.

Mweupe tu, ndiyo mweupe,
Ukiniosha nitakuwa safi.

Bwaba Yesu, unitazame sasa,
Unifanye niwe dhabihu hai;
Najitoa kwako, na moyo wote;
Unioshe sasa niwe mweupe.

Bwana kwa hiyo nakuomba sana,
Nakungojea miguuni pako,
Naomba unioshe damuni tu,
Unioshe sasa niwe mweupe.

Bwana nidumu kukungojea,
Niumbie moyo safi, Ee Mungu,
Wanaokujia hutupi kamwe,
Unioshe sasa niwe mweupe.

56.Ni siku kuu siku ile


Ni siku kuu siku ile
Ya kumkiri Mwokozi!
Moyo umejaa tele,
Kunyamaza hauwezi.

Siku kuu! Siku kuu!
Ya kuoshwa dambi zangu kuu!
Hukesha na kuomba tu,
Ananiongoza miguu.
Siku kuu! siku kuu!
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.

Tumekwisha kupatana
Mimi wake, yeye wangu,
Na sasa nitamwandama,
Nikiri neno la Mungu.

Moyo tulia kwa Bwana
Kiini cha raha yako,
Huna njia mbili tena;
Yesu ndiye njia yako.

Nadhiri yangu ya mbele
Nitaiweka daima,
Hata ije siku ile,
Ya kwonana kwa salama

58.Mwamba Wenye Imara


Mwamba wenye imara
Kwako nitajificha!
Maji hayo na damu
Yaliyotoka humu,
Hunisafi na dhambi,
Hunifanya mshindi.

Kwa kazi zote pia ,
Sitimizi sharia.
Nijapofanya bidii,
Nikilia nakudhii,
Hayaishi makosa;
Ndiwe wa kuokoa.

Sina cha mkononi,
Naja Msalabani;
Nili tupu, nivike;
Ni mnyonge, nishike;
Nili mchafu naja,
Nioshe nisijafa.

Nikungojapo chini,
Nakwenda kaburini;
Nipaapo Mbinguni,
Na kukwona enzini:
Roho yangu na iwe
Rahani mwako wewe.

57.Naendea Msalaba


Naendea Msalaba,
Ni mnyonge na mpofu,
Yapitayo naacha,
Nipone Msalabani.

Nakutumaini tu,
Ewe Mwana wa Mungu;
Nainamia kwako;
Niponye, mponya wangu.

Nakulilia sana:
Nalemewa na dhambi;
Pole Yesu asema;
“Nitazifuta zote”.

Natoa vyote kwako,
Nafasi nazo nguvu,
Roho yangu na mwili,
Viwe vyako milele.

Kwa damu yake sasa,
Nimegeuka roho,
Nikaziacha tama
Nimfuate Yesu tu.

Yesu yuaja tena!
Nimepevuka kwake,
Kila chembe kamili;
Msifuni yeye mponya!

60.Waponyeni Watu


Waponyeni watu wamo kifoni,
Watoeni walio shimoni;
Na aangukaye mumzuie;
Ya Bwana Yesu wahubirini.

Walio kifoni waokoeni,
Mwokozi yuko, wahubirini.

Wajapokawia anangojea,
Awasubiri waje tobani;
Msiwadharau, muwaonyeni;
Huwasamehe; wakiamini.

Myoyoni mwa ndani, yule shetani
Ameyaseta mawazo yao;
Lakini kwa Bwana huwa mazima,
Tukiwavuta kwa pole hao.

Kawaokoeni, wale njiani,
Mutimize mapenzi ya Bwana;
Na kwa nguvu zake warudi kwake,
Kwa subira waonyeni sana.

59.Peleleza Ndani Yangu


Peleleza ndani yangu,
Iwe safi nia,
Kwangu kama kwako Mungu,
Idhihiri pia.

Peleleza moyo wangu
Uunifunulie,
Yaliyomo ndani yangu
Nami niyajue.

Kwanza washe zako tambi,
Kumefunga giza;
Nijue ambavyo dhambi
Ni la kuchukiza.

Peleleza na mawazo
Ni mbegu za mambo,
Asili ya machukizo,
Maumbuo – umbo.

Zidi kuyapeleleza
Katikati yangu
Hata wishe nifundisha
Udhaifu wangu.

Hapo nikikwinamia
Mbele zako, Mungu,
Hakika nitakujua
U mpenzi wangu.

61.Tumesikia Mbiu


Tumesikia mbiu:
Yesu lo! aponya,
Utangazeni kote,
Yesu, lo! aponya.
Tiini amri hiyo;
Nchini na baharini,
Enezeni mbiu hii;
Yesu , lo! aponya.

Imbeni na vitani;
Yesu, lo! aponya;
Kwa nguvu ya kombozi,
Yesu, lo! aponya.
Imbeni wenye shida,
Unapoumwa moyo.
Na karibuni imba;
Yesu, lo! aponya.

Mawimbini uenee;
Yesu, lo! Aponya;
Wenye dhambi jueni;
Yesu, lo! Aponya.
Visiwa na viimbe,
Vilindi itikeni,
Na nchi shangilieni;
Yesu, lo! Aponya.

Upepo utangaze;
Yesu, lo! Aponya;
Mataifa yashangaaa;
Yesu lo! Aponya.
Milimani, bondeni,
Sauti isikike
Ya wimbo wa ushindi;
Yesu, lo! Aponya.

63.Ndugu wa kirohoni


Ndugu wa kirohoni
Mliokombolewa,
Tafakarini sana
Yatupasayo.

Wapenzi wake Yesu
Tuliokombolewa
Tujitoe kabisa
Wengi waponywe.

Siku itatimia
Tutakapoulizwa
Wale wa nyumba zetu
Na majirani

Tujitoeni, ndugu,
Tukahubiri Injili.
Atutumie Roho
kuponya wengi.

Wasiokombolewa
Ni wengi vijijini,
Wataokolewaje
Tukiogopa?

Bwana alijitoa
Akapotewa mengi,
Ili atuokoe,
Tusiwe waoga.

Aliyetununua,
Kwa kuimwaga damu,
Angalieni sana
Msimwepuke.

62.Bwana Wa Mabwana


Bwana wa mabwana,
Mwenye nguvu sana
Twakusihi:
Neno la milele
Na liende mbele,
Waongoke tele
Kwa Mwokozi.

Tunaowaona
Wanavyopatana,
Kulipinga,
Hawataliweza
Neno, kulitweza:
Huwaje! Kucheza:
Na upanga?

Heri wajitunze
Ili wapatane,
Na Mwokozi;
Watafute sana,
Wapate kuona,
Yesu kuwa Bwana,
Mkombozi.

Mungu awaita
Wasije kukuta
Pigo lake;
Hakuona vyema
Wakose uzima,
Awape rehema,
Waokoke.

Mwenye utukufu
Tunamshukuru
Yeye pweke!
Nasifiwe sana,
Baba, naye Mwana,
Na wa tatu tena
Roho yake.

64.Ujaribiwapo, Sifanye Dhambi


Ujaribiwapo, sifanye dhambi,
Bali uzishinde, kwa Yesu kutii.
Fuliza kiume ushinde tamaa;
Yesu ni Mwokozi, hukuokoa.

Umwombapo yu papo
Akuongeze nguvu,
Atakusaidia;
Yesu atakufaa.

Wepushe waovu, matusi dharau;
Heshima la Mungu, kamwe sisahau;
Fanya uhodari, uwe mpole,
Atakuokoa hata milele.

Avumiliaye hupewa taji;
Tujaposumbuka tu washindaji,
Na mwokozi wetu hutuwezesha
Tusiwe kushindwa kama twakesha.

66.Po Pote Mashamba Yajaa


Po pote mashamba yajaa,
Tele nafaka pevu,
Po pote yang’aa meupe
Bondeni na nyandani.

Mwenye mavuno, wasihi
Upeleke wavuni,
Wakusanye mazao,
Hata kazi iishe.

Wapeleke uchaoni,
Waende na jotoni,
Mpaka jua lishukapo
Wakusanye ko kote.

Watenda kazi wa Bwana,
Mlete sasa mazao,
Na jioni ingieni
Kwake na furaha kuu.

65.Safari


Katika safari yetu
Kwenda Mbinguni
Tusiishe siku zetu
Usingizini.

Ng’oani! Tujifungeni,
Twende zetu juu!
Kristo ndiye kiongozi;
Tusihofu tu.

Atwekwe badala yetu,
Mwenyewe Bwana;
Yesu kiongozi wetu
Atapokea.

Kisimani, maji tele,
Maji mazima!
Maji hayo,
Ya milele
Yana neema.

Njiani miiba mingi,
Yatuumiza;
Hofu na hatari nyingi,
Sana zakaza.

Kweli, njia ya Mbinguni
Ni ya mashaka;
Tuwe na Yesu njiani,
Mara hufika.

67.Bwana Uliyewaita


Bwana uliyewaita
Watakatifu wako,
Wawe mitume, wachunga,
Walishe kundi lako;
wanyonge na wenye hofu
Wakawa mashujaa,
Na wapole wa kunena
Wasiwe kunyamaa.

Hata leo wawataka
Watakatifu wako,
Nawe wauliza tena
Ni nani aliyeko
Atakaye nimtume
Afundishe vijana?
“Ni tayari, Bwana wangu,
Nitume mimi Bwana.”

Nitume na mimi, Bwana
Kama ulivyotumwa,
Habari ya msamaha
Na dhambi kutubiwa,
Niwahubiri wakosa,
Na waliopotea,
Wokovu u wake Bwana,

Aliyewafilia.
Astahiliye hapana
Kutamka habari,
Lakini wewe waweza
Kutufanya tayari.
Neno lako tulijue,
Tupe na roho yako,
Hayatakuwa ya bure,
Haya maneno yako.

69.Twendeni Askari


Twendeni askari, watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele, tumwandame juu.
Ametangulia Bwana vitani,
Twende mbele kwani ndiye amini.

Twende askari watu wa Mungu;
Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.

Jeshi la Shetani, likisikia
Jina la Mwokozi, litakimbia,
Kelele za shangwe zivume nchi;
Ndugu inueni zenu sauti.

Kweli kundi dogo, watu wa Mungu
Sisi na mababa tu moja fungu.
Hatutengwi nao, moja imani,
Tumaini moja, na moja dini.

Haya mbele watu nasi njiani,
Inueni myoyo, nanyi sifuni;
Heshima na sifa ni ya Mfalme,
Juu hata chini, sana zivume.

68.Mungu Msaada Wetu


Mungu msaada wetu
Tangu myaka yote,
Ndiwe tumaini letu
La zamani zote.

Kivuli cha kiti chako
Ndiyo ngome yetu.
Watosha mkono wako
Ni ulinzi wetu.

Kwanza havijakuwako
Nchi na milima,
Ndiwe Mungu; chini yako
Twakaa salama.

Na myaka elfu ni kama
Siku moja kwako;
Utanilinda daima
Tu wenyeji wako.

Binadamu huondoka,
Mwisho hana kitu;
Kama ndoto hutoweka
Ndivyo hali yetu.

Ila wewe Mungu wetu
Ndiwe wa kudumu;
Ndiwe bora, ngome yetu
Twakaa dawamu.

70.Yesu Atuchunga


Yesu atuchunga,
Mchunga wetu,
Naye atufuta
Machozi yetu;
Mkononi mwake
Hatuna hofu,
Daima twapata
Kwake wokovu.

Yesu atuchunga
Tumemjua,
Na sauti yake
Twaitambua;
Naye akituonya
Ni kwa upole,
Tu kondoo zake
Hata milele.

Yesu atuchunga;
Aliwafia
Kondoo wakubwa
Na wana pia;
Kwamba awajua,
Kondoo zake,
Hutiwa alama
Ya damu yake.

Yesu atuchunga;
Mikono yake
Imewaambata
Kondoo zake;
Hapati wadhuru
Adui yule,
Yesu awalinda.

72.Twendeni! Haraka!


Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno
Liwe mwanga kwa nchi zilizo giza.
Bwana alisema nendeni po pote
Kawafundisheni mataifa yote.
Pelekeni Injili kwa jina la Yesu.
Upesi! Twendeni haraka!

Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno
La upendo wa Mungu kwa watu wote;
Aliyeupenda sana ulimwengu
Akamtoa Yesu Mwana wake pekee
Kaleta wokovu, tumtangazeni.
Upesi! Twendeni haraka!

Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno
La uzima kwa watu waliokufa.
Mateka ya Shetani litafungua
Litaponyesha na kuwapa amani.
Twendeni upesi, tukawaokoe.
Upesi! Twendeni haraka!

71.Mteteeni Yesu


Mteteeni Yesu,
Mlio askari;
Inueni beramu,
Mukae tayari,
Kwenda nae vitani,
Sisi hatuchoki
Hata washindwe pia
Yeye amiliki.

Mteteeni Yesu,
Vita ni vikali;
Leo siku ya Bwana,
Atashinda kweli,
Waume twende naye,
Adui ni wengi,
Lakini kwake Bwana
Tuna nguvu nyingi.

Mteteeni Yesu,
Wenye ushujaa;
Nguvu zenu za mwili
Hazitatufaa;
Silaha ya injili
Vaeni daima,
Kesheni mkiomba,
Sirudini nyuma.

Mteteeni Yesu,
Vita ni vikali,
Wengi wamdharau,
Hawamkubali,
Ila atamiliki
Tusitie shaka,
Kuwa naye vitani
Twashinda hakika.

73.Yesu Zamani Bethrehemu


Yesu zama Bethrehemu,
Aliyezaliwa kwa aibu,
Ndiye mwakozi wa ulimwengu,
Akaja kwa mimi.

Akaja kwa mimi; akaja kwa mimi;
Ndiye mwaokozi wa ulimwengu,
Akaja kwa mimi.

Yesu akafa msalabani,
Kuniponya akalipa deni,
Ni la ajabu ya jinsi gani
Kunifia mimi!

Kunifia mimi! Kunifia mimi!
Ni la ajabu ya jinsi gani
Kunifia mimi.

Ni yeye huyo tangu asili;
Na nilipotanga-tanga mbali
Alikuja kwa upole, kweli
Kuniita mimi.

Kuniita mimi; Kuniita mimi;
Alikuja kwa upole, kweli
Kuniita mimi

Yesu kristo atarudi tena,
Hilo lanifurahisha sana.
Yeye Bwana akionekana
Kunijia mimi.

Kunijia mimi, kunijia mimi,
Yeye Bwana akionekana
Kunijia mimi

74.Wachunga Walipolinda


Wachunga walipolinda
Kucha nyama zao,
Malaika mtukufu
Alishuka kwao.

Wakacha sana wachunga,
Akawatuliza,
“Nawaletea habari
Ya kuwapendeza.”

”Mji ule wa Daudi
Leo amezawa
Mwokozi ni Kristo Bwana,
Ilivyoandikwa”.

”Huyo mwana wa Mbinguni
Ataonekana,
Amelazwa kihorini
Malazi hapana.”

Alipokwisha yanena
Malaika hao
Waliimba wimbo huu
Usio na mwisho:

”Enzi ni yake Munju juu,
Na nchi salama,
Kwa watu nao radhi kuu,
Sasa na daima.”

75.Waimba, Sikizeni


Waimba, sikizeni,
Malaika Mbinguni;
Wimbo wa tamu sana
Wa pendo zake Bwana,
“Duniani salama,
Kwa wakosa rehema.”
Sisi sote na twimbe
Nao wale wajumbe;
Waimba, sikizeni,
Malaika mbinguni.

Ndiye Bwana wa Mbingu,
Tangu milele Mungu,
Amezaliwa mwili,
Mwana wa mwanamwali;
Ametoka enzini
Kuja ulimwenguni
Mwokozi atufie,
Ili tusipotee.
Waimba, sikizeni,
Malaika Mbinguni.

Mtukufu wa amani
Ametoka Mbinguni,
Jua la haki, ndiye
Atumulikiaye;
Amejivua enzi,
Alivyo na mapenzi,
Ataka kutuponya,
Kutuzalisha upya,
Waimba sikizeni,
Malaika Mbinguni.

Njoo upesi, Bwana,
Twakutamani sana;
Kaa nasi, mwokozi
Vita hatuviwezi;
Vunja kichwa cha nyoka,
Sura zako andika,
Tufanane na wewe,
Kwetu sifa upewe,
Waimba, sikizeni,
Malaika Mbinguni.

76.Njoni Enyi Wa Imani


Njoni na furaha, enyi wa imani,
Njoni Bethilehemu upesi !
Amezaliwa jumbe wa Mbinguni;
Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
Njoni tumuabudu Mwokozi.

Mungu wa waungu, Mwanga wa mianga,
Amekuwa radhi kuzaliwa;
Mungu wa kweli, wala si kiumbe;
Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
Njoni tumuabudu Mwokozi.

Jeshi la Mbinguni, Imbeni kwa nguvu,
Mbingu zote na zijae sifa;
Sifuni Mungu aliye Mbinguni;
Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
Njoni tumuabudu Mwokozi.

Ewe Bwana mwema, twakubarikia,
Yesu, utukufu uwe wako;
Neno la Baba limekuwa mwili;
Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
Njoni tumuabudu Mwokozi.

78.Sioshwi Dhambi Zangu


Sioshwi dhambi zangu,
Bila damu yake Yesu.
Hapendezewi Mungu,
Bila damu yake Yesu.

Hakuna kabisa
Dawa ya makosa
Ya kututakasa,
Ila damu yake Yesu.

La kunisafi sina
Ila damu yake Yesu.
Wala udhuru tena,
Ila damu yake Yesu.

Sipati pataniswa,
Bila damu yake Yesu.
Hukumu yanitisha,
Bila damu yake Yesu.

Sipati tumaini,
Bila damu yake Yesu.
Wema wala amani,
Bila damu yake Yesu.

Yashinda ulimwengu,
Hiyo damu yake Yesu.
Na kutufikisha juu,
Hiyo damu yake Yesu.

Twaimba: Utukufu
Una damu yake Yesu.
Milele twaisifu,
Hiyo damu yake Yesu.

77.Msalabani Pa Mwokozi


Msalabani pa mwokozi,
Hapo niliomba upozi,
Akaniokoa mpenzi,
Mwana wa Mungu.

Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.

Chini ya mti msumbufu,
Niliomba utakatifu,
Alinikomboa kwa damu,
Mwana wa Mungu.

Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu.

Aliniokoa dhambini,
Ikawa kunikaa ndani,
Aliponifia mtini,
Mwana wa Mungu.

Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Aliponifia Mtini, Mwana wa Mungu.

Damu ya Yesu ya thamani,
Huniokoa makosani,
Huniendesha wokovuni,
Mwana wa Mungu.

Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Huniendesha wokovuni, Mwana wa Mungu.

Hicho kijito cha gharama,
Leo jivike kwa kuzama,
Kwake uuone uzima,
Mwana wa Mungu.

Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Kwake uuone uzima, Mwana wa Mungu.

80.Wamwendea Yesu kwa kusafiwa


Wamwendea Yesu kwa kusafiwa,
Na kuoshwa kwa damu ya kondoo?
Je neema yake umemwagiwa,
Tumeoshwa kwa damu ya kondoo?

Kuoshwa, kwa damu,
Itutakasayo ya kondoo;
Ziwe safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa kwa damu ya kondoo?

Wamwandama daima mkombozi
Na kuoshwa na damu ya kondoo?
Yako kwa msulubiwa makazi,
Umeoshwa kwa damu ya kondoo?

Atakapokuja Bwana –arusi
Uwe safi kwa damu ya kondoo!
Yafae kwenda mbinguni mavazi
Yafuliwe kwa damu ya kondoo.

Yatupwe yaliyo na takataka,
Na uoshwe kwa damu ya kondoo.
Huoni kijito chatiririka
Na uoshwe kwa damu ya kondoo?

79.Msalaba Wa Aibu


Msalaba wa aibu,
Ulinipa amani;
Uliniondoa kifungoni,
Nilimotesekea.

Ee, Mwokozi wangu, Yesu
Nitamwendea nani?
Najiweka msalabani,
Nikaoshwe damuni.

Nakupenda Bwana Yesu,
Kwa kunipenda kwako,
Napendezwa nikutumikie
Maisha yangu yote.

Usifiwe Bwana Yesu,
Kwa ulivyonifia,
Aleluya, nakushukuru,
Uliyenikomboa.

Msalaba ulishinda
Nguvu zake adui,
Ili mimi nikombolewe,
Niwe mwana wa Mungu.

Wednesday, December 7, 2016

⁠⁠⁠81.Chini Ya Msalaba


Chini ya msalaba
Nataka simama;
Ndio mwamba safarini,
Wa kivuli chema;
Ni kweli kwa roho yangu
Ni tuo kamili,
Tatua mzigo wangu
Wakati wa hari.

Hapa ni pema sana,
Ni ngome kamili;
Hapa yameonekana,
Mapenzi ya kweli;
Kama alivyoonyeshwa
Yakobo zamani,
Msalaba umekuwa
Ngazi ya Mbinguni.

Na Yesu msalabani
Walimkemea,
Alikufa niokoke
Niliyepotea;
Naona ajabu sana
Ya mambo mawili
Jinsi alivyonipenda,
Nisiyestahili.

Atakayeonana,
Na Yesu Mbinguni,
Njia yake aanzapo
Ni msalabani;
Wokovu upo hapa tu,
Mwingine hapana,
Kisha kuna furaha kuu
Pamoja na Bwana.

82.Sioni haya kwa Bwana


Sioni haya kwa Bwana
Kwake nitang’ara!
Mti wake sitakana,
Ni neno imara!

Msalaba ndio asili ya mema,
Nikatua mzigo hapo;
Nina uzima, furaha daima,
Njoni kafurahini papo.

Kama kiti chake vivyo
Ni yake ahadi,
Alivyowekewa navyo
Kamwe havirudi.

Bwana wangu, tena Mungu
Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu
Wala kunikana.

Atakiri langu jina,
Mbele za Babaye,
Anipe pahali tena
Mbinguni nikae.

84.Niwonapo Mti Bora


Niwonapo mti bora
Kristo aliponifia
Kwangu pato ni hasara
Kiburi nakichukia.

Na nisijivune, Bwana
Ila kwa mauti yako;
Upuzi sitaki tena,
Ni chini ya damu yako.

Tangu kichwa hata nyayo,
Zamwagwa pendo na hamu,
Ndako pweke hamu hiyo,
Pendo zako zimetimia.

Vitu vyote vya dunia,
Si sadaka ya kutosha;
Pendo zako zinawia
Nafsi, mali, na maisha.

83.Kwa Wingi Wa Nyama


Kwa wingi wa nyama,
Na sadaka pia,
Hupata wapi salama,
Kwondoa hatia?

Sadaka ni Yesu,
Hwondoa makosa;
Dhabihu mwenye jina kuu,
Atanitakasa.

Kwa yangu imani,
Nikuweke sasa
Mkono mwako kichwani
Kukiri makosa.

Roho yakumbuka
Mambo ya mtini,
Mzigo ulijitweka,
Ndiyo yangu deni.

Deni hutanguka,
Tukimuamini;
Kwa damu tumeokoka,
Twimbe furahani.

85.Ni “Mtu Wa Simanzi


Ni “Mtu wa Simanzi”,
Mwana wa mwenye enzi
Mwenye mengi mapenzi!
Asifiwe Bwana Yesu!

Akawa matesoni,
“Mungu mwana yakini
Akatoka Mbinguni:
Asifiwe Bwana Yesu!

Akapata dhihaka,
Mzoea – mashaka
Ndiye yetu sadaka:
Asifiwe Bwana Yesu!

Tu wenye dhambi sana;
Kwake dhambi hamna,
Na Mungu twapatana:
Asifiwe Bwana Yesu!

Alikufa mtini,
Akalia dhikini,
Sasa yuko Mbinguni:
Asifiwe Bwana Yesu!

Punde atarejea,
Yesu kutunyakua,
Ndipo tutamwimbia:
Asifiwe Bwana Yesu!

86.Damu Imebubujika

Damu Imebubujika,
Ni ya Imanweli,
Wakioga wenye taka,
Husafiwa kweli.

Ilimpa kushukuru
Mwivi mautini;
Nami nisiye udhuru,
Yanisafi ndani.

Kondoo wa kuuawa,
Damu ina nguvu,
Wako wote kuokoa,
Kwa utimilivu.

Bwana tangu damu yako
Kunisafi kale,
Nimeimba sifa zako;
Taimba milele.

Nikifa tazidi kwimba
Sifa za wokovu
Ulimi ujaponyamaa
Vumbini mwa ufu.

Bwana, umenikirimu
Nisiyestahili
Kwa damu yako, sehemu
Ya mali ya kweli.

Nikubali kukwimbia,
Mbinguni milele,
Mungu nitakusifia
Jina lako pweke.

87.Deni Ya Dhambi Ilimalizika


Deni yangu ya dhambi,
Yesu amelipa.
Kwake msalabani
Nilipewa uzima.

Deni ya dhambi,
Msalabani,
Ilimalizikia,
Ni huru kabisa.

Bwana Yesu asema,
“Mwanangu dhaifu,
Uwezo wa ushindi
Hupatikana kwangu.”

Bwana, kweli naona,
Nguvu zako pekee
Huondoa ukoma,
Niwe kipya kiumbe.

Sina wema moyoni,
Nidai neema,
Nakubali kabisa,
Kwa damu kusafiwa.

Hata huko Mbinguni
Miguuni pake,
“Yesu alinifia,”
Nitaimba milele.

89.Kwa Kalvari


Muda mwingi nilipotea,
Sikufahamu msalaba,
Wala aliyenifilia,
Kwa Kalvari.

Rehema bure na neema,
Samaha nalo nilipewa,
Ndipo aliponifungua
Kwa Kalvari.

Kwa neno lake Bwana Mungu,
Nilijiona mimi mwovu,
Nikageuka na kutubu,
Kwa Kalvari.

Yote kwa Yesu namtolea,
Ndiye mfalme wa pekee sasa,
Kwa furaha nitamwimbia,
Wa Kalvari.

Jinsi pendo lilivyo kuu,
Neema ilishuswa toka juu,
Alitufanyia wokovu
Kwa Kalvari.

88.Ndiyo Damu ya Baraka


Ndiyo damu ya baraka ituoshayo wakosa,
Kwake Bwana twaokoka, nasi twamsifu sasa;
Nimestahili hukumu, siwezi kujitakasa;
Nioshe katika damu, takuwa safi kabisa.

Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe katika damu;
Takuwa safi kabisa.

Yesu alivikwa miiba, na kuangikwa Mtini,
Na maumivu si haba yaliyompata chini.
Nataka kijito hicho niende kuoga sasa;
Ndicho kinitakasacho, nami ni safi kabisa.

Safi kabisa; safi kabisa!
Ndicho kinitakasacho,
Nami ni safi kabisa.

Baba, kweli nimekosa, moyo wangu ni dhaifu;
Dhambi ni nyingi kabisa, nipate wapi wokovu?
Yesu kijitoni pako, naja naamini sasa;
Nioshe kwa damu yako, takuwa safi kabisa.

Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe kwa damu yako,
Nami ni safi kabisa.

91.Mapenzi Yako Yafanyike Bwana


Mapenzi yako yafanyike,
Wewe mfinyanzi, nami towe,
Unifinyange upendavyo,
Mimi tayari, naja kwako.

Mapenzi yako yafanyike,
Unihoji dhambi zote,
Unisafishe vya kimwili,
Niinamapo Msalabani.

Mapenzi yako yafanyike,
Mimi dhaifu, mimi mnyonge.
Uwezo wote, kwako kweli,
Sasa niponye, Ee, Mwokozi.

Mapenzi yako yafanyike,
Natoa kwako vitu vyote,
Maisha, mali, moyo, mwili,
Vyote ni vyako, kweli, kweli.

Mapenzi yako yafanyike,
Mapenzi yangu yavunjike,
Ninakubali uwe Bwana,
Ni mali yako, twaa kabisa.

Mapenzi yako yafanyike,
Unitawale siku zote,
Sura ya Yesu umba kwangu,
Nijaze Roho nayo nguvu.

90.Aliteswa, Aliteswa


Aliteswa, aliteswa,
Msalabani Yesu aliteswa,
Dhambi zangu ameziondoa,
Mahali pangu aliumizwa.

Alikufa, alikufa,
Msalabani Yesu alikufa,
Kwa kifo chake nakombolewa,
Kwa kuwa Yesu alinifia.

’Kafufuka, ‘kafufuka,
Kaburini Yesu alitoka,
Nami nimewekwa huru pia,
kwa kuwa Yesu alifufuka.

Yuko hai, yuko hai,
Mbinguni anaishi Mwombezi,
Daima huniombea mimi,
Kwa kuwa Yesu adumu hai.

Atarudi, atarudi,
Siku moja Yesu atarudi,
Na tutamwonapo tutafurahi,
Kwa kupelekwa kwake Mbinguni.

Sifa kwake, sifa kwake,
Mbinguni na huimbwa milele,
Kwa furaha, masifu, na shangwe,
Tutamwimbia Yesu milele.

92.Nataka Nimjue Yesu


Nataka nimjue Yesu,
Na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake, na
Wokovu wake kamili.

Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue pendo lake, na
wokovu wake kamili.

Nataka nione Yesu,
Na nizidi kusikia,
Anenapo kitabuni,
Kujidhihirisha kwangu.

Nataka nifahamu, na
Nizidi kupambanua
Mapenzi yake, nifanye
Yale yanayompendeza.

Nataka nikae naye,
Kwa mazungumzo zaidi,
Nizidi kuwaonyesha
Wengine wokovu wake.

94.Siku Ya Mbingu Kujawa Na Nifa


Siku ya Mbinguni kujawa na sifa,
Dhambi zilizidi duniani;
Yesu akaja azaliwe mtu,
Awe na watu ulimwenguni.

Alinipenda, alinifia,
Ameondoa na dhambi zangu;
Alifufuka nipewe haki,
Yuaja tena Mwokozi wangu.

Na siku moja walikwenda naye,
Wakamkaza msalabani;
Aliumia, aliaibishwa,
Ili atuokoe dhambini.

Siku hiyo wakamlaza chini
Kaburini alipumzika;
Matumaini yetu wenye dhambi,
Ni mwokozi, kwake twaokoka.

Kaburi likashindwa kumshika;
Jiwe likatoka mlangoni,
Alifufuka kwa kushinda kwake,
Naye yuko milele Mbinguni.

Siku moja atatujia tena;
Utukufu wake tutaona;
Atawaleta na wapenzi wetu;
Mwokozi: wangu, tutaonana.

93.Bwana Amefufuka


Bwana amefufuka, Aleluya.
Twimbe na malaika, Aleluya.
Sifa zetu na shangwe, Aleluya.
Na zao zisitengwe, Aleluya.

Ukombozi timamu, Aleluya.
Umetimu kwa damu, Aleluya.
Mshindi asifiwe, Aleluya.
Yu hai kwa milele. Aleluya.

Jiwe, lindo, muhuri, Aleluya.
Vi wapi? Na kaburi? Aleluya.
Kifo hakimuweki, Aleluya.
Ametoka peponi, Aleluya.

Yu hai mtukufu; Aleluya.
Cha kifo hatuhofu! Aleluya.
Alitufia sisi, Aleluya.
Tuwe mahuru nasi, Aleluya.

Kichwa chatangulia, Aleluya.
Tupae, nasi, pia!, Aleluya.
Kwa kuwa tuna fungu, Aleluya.
Mti, kaburi, mbinguni, Aleluya.

Ndiwe Mwokozi wetu, Aleluya.
Sifa ni yako Yesu, Aleluya.
Utukuzwe pekeo, Aleluya.
Ni wewe ufufuo, Aleluya.

96.Mle kaburini, Yesu Mwokozi!


Mle kaburini, Yesu Mwokozi!
Alilazwa chini, Bwana wangu!

Bwana! Amefufuka,
Kifo kimeshindwa kabisa!
Gizani mle alitoka chini,
Sasa atawala huko Mbinguni!
Yu hai! Yu hai!
Bwana Yesu yu hai!

Aungoja huo, Yesu Mwokozi!
Mchana ujao, Bwana wangu!

Walinda kaburi, Yesu Mwokozi!
Bure ni muhuri, Bwana wangu!

Kifo kimeshindwa, Yesu mwokozi!
Pingu zimevunjwa, Bwana wangu!

95.Hivi vita, vimekoma


Aleluya! Aleluya! Aleluya!

Hivi vita vimekoma,
Vimeshindwa na uzima,
Na asifiwe daima,
Bwana Yesu.

Nguvu za kifo ni hizo,
Ila hazina uwezo,
Ndizo sasa avunjazo,
Bwana Yesu.

Siku tatu za huzuni,
Kisha atoka ufuni,
Asifiwe duniani,
Bwana Yesu.

Mapingu ameyavunja,
Mbingu amezifungua,
Nasi sasa twamwimbia,
Bwana Yesu.

Na ulivyopigwa wewe,
Ni kwamba tufunguliwe,
Milele na usifiwe,
Bwana Yesu.

97.Tazameni Huyo Ndiye


Tazameni huyo ndiye,
Mwenye kushinda vita;
Haya, tumsujudie;
Nyara anazileta;
Watu wote msifuni,
Sasa yumo kitini.

Msifuni malaika,
Mtukuzeni sana,
Wote waliookoka
Watamsifu Bwana;
Watu wote msifuni,
Sasa yumo kitini.

Walimfanya dhihaka
Zamani wenye shari,
Kwao waliookoka
Ni Bwana wa fahari;
Watu wote msifuni.
Sasa yumo Kitini.

Nyimbo nzuri, sikizeni,
Ni nyimbo za sifa kuu,
Za Bwana Yesu kitini,
Kutawazwa, yeye tu;
Watu wote msifuni
Sasa yumo Kitini.

Tuesday, December 6, 2016

98.Huyo Ndiye! Anashuka


Huyo ndiye! anaskuka,
Aliyetufilia,
Wengi waliookoka,
Wakimfurahia,
Aleluya!
Yesu aturudia.

Sote tutamtazama,
Amekaa kitini,
Nao waliomcoma,
Kumkaza mtini,
Na kilio, wamuone enzini.

Alama za kifo chake
Hata sasa anazo
Na waaminifu wake
Wapendezewa nazo.
Alipata,
Kwetu alama hizo.

Wokovu utakiwao
Sasa wapatikana,
Na watakatifu hao
Mbinguni wakutana
Kumlaki,
Ndiyo siku ya Bwana

Wakusujudie wote
Mbele ya kiti chako.
Zako, Bwana, nguvu zote
Itwae milki yako
Njoo Bwana,
Sisi tu watu wako.

100.Tumrudie Bwana


Mbona washangaa njiani?
Mbona warejea nyuma?
Warudi tena gizani
Alimokutoa Bwana?

Ni ya bure yote haya,
Uliyofunzwa ya Mungu?
Ni bure amekufia
Bwana Yesu kwa uchungu?

Wamtia kristo aibu
Na maneno yake pia?
Siku yaja ya hesabu,
Utamjibuje Bwana?

Upandapo tena hayo,
Halafu utayavuna.
Rudi kwa Bwana upesi,
Mwombe akupokee tena.

99.Maelfu Na Maelfu


Maelfu na maelfu
Wenye nguo bora!
Masafu ya waongofu
Wenye na bendera!
Amekwisha kamili
Vita vya shetani
Fungueni lango hili;
Njoni, ingieni!

Imbeni aleluya,
Zipae Mbinguni!
Pigeni sana sauti
Kwa kutumaini!
Kwa hiyo viliumbwa
Nchi hata Mbingu
Dhiki za muda zikisha,
Asifiwe Yesu.

Loo! Tukionana
Pwani ya ng’amboni!
Loo! Tukishirikiana
Milele Mbinguni!
Midomo yote pia,
Huko itaimba
Wajane kufufukiwa
Na kila yatima!

Himiza enzi yako,
Uliyetufia
Utimize watu wako,
Wakosaji pia,
Mpendwa wa taifa
twakutumaini!
Uzifunue ishara
Urudi enzini!

101.Twonane Milele


Nyimbo na tuziimbe tena
Za alivyotupenda mbele;
Kwa damu ya thamani sana!
Mbinguni twonane milele.

Twonane milele,
Twonane bandarini kule;
Twonane milele,
Twonane bandarini kule.

Hupozwa kila aoshwaye,
Kwa damu ya Kondoo yule;
Ataishi afurahiye
Vya Yesu mbinguni milele.

Hata sasa hufurahia
Tamu yake mapenzi yale,
Je, kwake tukifikilia,
Kutofarakana milele?

Twende mbele kwa jina lake,
Hata aje mwokozi yule,
Atatukaribisha kwake,
Tutawale naye milele.

Sauti zetu tuinue
Kumsifu Mwokozi yule,
Ili watu wote wajue
Wokovu u kwake milele.

103.Kaa Nami


Kaa nami, ni usiku tena;
Usiniache gizani, Bwana;
Msaada wako haukomi;
Nili peke yangu, kaa nami.

Siku zetu hazikawi kwisha,
Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho hakikomi,
Usiye na mwisho kaa nami.

Nina haja nawe kila saa;
Sina mwingine wa kunifaa;
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe? Bwana, kaa name.

Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote, si taabu;
Kifo na kaburi haviumi;
Nitashinda kwako, kaa nami.

Nilalapo nikuone wewe,
Gizani mote nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi,
Siku zangu zote kaa nami.

102.Kazi Yangu Ikiisha


Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka;
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua Mwokozi nifikapo ng’amboni;
Atakuwa wa kwanza kunilaki.

Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

Furaha nitapata nikiona makao
Bwana aliyotuandalia;
Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyonipa pahali Mbinguni.

Nao waliokufa katika Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni,
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha,
Pasipo machozi wala huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele; lakini
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

104.Twasoma Ni Njema Sana


Twasoma, ni njema sana
Mbinguni, kwa Bwana;
Twasoma, dhambi hapana,
Mbinguni kwa Bwana;
Malaika wema wako,
Vinanda vizuri viko,
Na majumba tele yako,
Mbinguni kwa Bwana.

Siku zote ni mchana,
Ni nchi ya raha;
Wala machozi hapana,
Ni nchi ya raha;
Walioko wanuona
Uso wa Mwokozi, tena
Jua jingine hapana,
Ni nchi ya raha.

Nyama na vitu viovu
Havimo kabisa;
Kifo nacho, na ubovu,
Havimo kabisa.
Ni watakatifu wote,
Wameoshwa dhambi zote;
Wasiosafiwa wote
Hawamo kabisa.

Tuna dhambi, pia sote,
Mwokozi akafa;
Kwake tutaoshwa zote,
Mwokozi akafa;
Kwake twapata wokovu,
Tutawona utukufu;
Mbinguni tutamsifu;
Mwokozi akafa.

Baba, mama, ndugu zetu,
Twendeni kwa Bwana;
Huku chini sio kwetu,
Twendeni kwa Bwana;
Tusishikwe na dunia,
Na dhambi kutulemea;
Tutupe vya chini pia,
Twendeni kwa Bwana.

105.Kuwatafuta


Kuwatafuta wasioweza,
Kuomba wamrejee Yesu,
Kuwaambia maneno yake,
“Njooni kwangu, nawapenda”.

Nitakwenda, (kwenda), niwatafute
Waongofu (wa Bwana) wageuke,
Waingie (wote) katika zizi
La Mkombozi (wetu) Yesu kristo.

Kuwatafuta wasioweza,
Waonyeshwe Mwokozi wetu,
Kuwaongoza, wapate wote
Uzima wa milele.

Kazi hiyo nataka kufanya,
Leo nimesikia mwito
Kuwainua waangukao,
Waletwe kwake Yesu njia.

107.Ewe,Baba Wa Mbinguni


Ewe, Baba wa Mbinguni,
Usikie twombalo
Hapa chini duniani,
Na uwe radhi nalo

Ee Mungu, bariki
Ndugu hawa wawili!
Ee Mungu, bariki
Ndugu hawa wawili!

Watu hawa mbele zako,
Na mbele ya kanisa;
Watimize Neno lako
Wanakutana sasa.

Kama Yesu na Kanisa,
Ni mmoja, na hivyo,
Watu hawawape sasa
Wawe mmoja vivyo

Walinde, Bwana, daima,
Wabariki nyumbani
Uwape nyingi salama
Humu ulimwenguni.

Wabariki, ewe Bwana,
Watu hawa wawili,
Wape upaji wa wana,
Wafurahishwe kweli.

Siku za duniani
Zitakapopungua,
Wape kurithi Mbinguni
Mema ya kwendelea.

106.Mungu Awe Nanyi Daima


Mungu awe nanyi daima,
Hata twonane ya pili,
Awachunge kwa fadhili,
Mungu awe nanyi daima.

Hata twonane huko juu,
Hata twonane kwake kwema;
Hata twonane huko juu,
Mungu awe nanyi daima.

Mungu awe nanyi daima;
Ziwafunike mbawaze,
Awalishe, awakuze;
Mungu awe nanyi daima.

Mungu awe nanyi daima;
Kila wakati wa shani
Awalinde hifadhini;
Mungu awe nanyi daima.

Mungu awe nanyi daima;
Awabarikie sana,
Awapasulie kina;
Mungu awe nanyi daima.

108.Twenenda Sayuni


Mpendao Bwana
Ije raha yenu!
Imbeni nyimbo za raha
Wa ibada yenu.

Twenenda Sayuni,
Mji mzuri Sayuni;
Twenenda juu Sayuni
Ni maskani ya Mungu.

Wasiimbe wao
wasioamini,
Watoto wa Mungu ndio
waimbao chini.

Twaona rohoni
Baraka za Mungu,
Tusijafika Mbinguni
Kwenye utukufu.

Tutakapo mwona
Masumbuko basi,
Huwa maji ya uzima,
Anasa halisi.

Tupaaze sauti,
Na fute machozi,
Twenenda kwa Imanweli
Naye ni Mwokozi.

110.Mapya Ni Mapenzi Hayo


Mapya ni mapenzi hayo,
Asubuhi tunayo,
Saa za giza hulindwa
Kwa uzima kuamshwa.

Kila siku, Mapya pia
Rehema, wema, na afya,
Wokofu, na msamaha,
Mawazo mema, furaha.

Tukijitahidi leo
Na mwendo utupasao,
Mungu atatueleza
Yatakayompendeza.

Mambo yetu ya dunia
Mungu atayang’aria,
Matata atageuza
Yawe kwetu ya Baraka.

Yaliyo madogo, haya
Mungu tukimfanyia,
Yatosha: tutafaidi
Huvuta kwake zaidi.

Ewe Bwana, siku zote,
Tusaidie kwa yote:
Mwendo wetu wote vivyo,
Uwe kama tuombavyo.

109.Nitaimba Na Yesu


Nitaimba ya Yesu,
Kwa rehema zake,
Baraka nyingi sana
Nimepata kwake;
Nitaimba ya Yesu,
Sadaka ya Mungu,
Alimwaga damu
Ukombozi wangu.

Nitaimba ya Yesu
Hapa siku zote,
Nitakapokumbuka
Vyema vyake vyote;
Nitaimba ya Yesu
Hata mashakani,
Yeye atanilinda
Mwake ubavuni.

Nitaimba ya Yesu
Niwapo Njiani;
Takaza Mwendo, hata
Nifike Mbinguni;
Nikiisha ingia
Mlangoni mle,
Yesu nitamwimbia
Mbinguni milele.

112.Nilikupa Wewe, Maisha Yangu


Nilikupa wewe
Damu ya moyoni,
Ili wokolewe,
Winuke ufuni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

Nilikupa miaka
Yangu duniani
Upate inuka,
Kuishi Mbinguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini:

Niliacha nuru
Za Baba, Mbinguni,
Kwingia taabu
Za ulimwenguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

Niliteswa sana,
Mateso kifoni,
Usije yaona
Hayo ya motoni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

Nimekuletea
Huku duniani
Upendo na afya
Zatoka Mbinguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

Nipe siku zako,
Udumu mwangani;
Na taabu yako,
Wingie rahani
Nafsi, pendo, mali,
Twae Imanweli.

111.Neno,Lako Bwana


Neno lako, Bwana,
Ni imara sana;
Lilo latwongoza,
Lilo latufunza.

Adui wabaya
Wakikaribia,
Neno lake Bwana
Ni ulinzi sana.

Siku za dhoruba
Soma ukiomba;
Neno lake Bwana
Msaada sana.

Ukiliamini,
Hwenda na amani;
Una na furaha
Neno ni siraha.

Ni furaha kweli,
Na wingi wa mali,
Neno lake Bwana
Kwa wasiokana

Neno la rehema,
Tukali wazima;
Faraja I papo,
Tufarikanapo.

113.Ni Mfalme Wa Mapenzi


Ni Mfalme wa mapenzi
Ndiye anichungaye,
Sipungukiwi, hawezi.
Kunipoteza yeye.

Kando ya mji mazima
Yeye huniongoza
Katika malisho mema
Daima hunilaza.

Mara nyingi hupotea
Kwa ukaidi wangu,
Naye huniandamia,
Hunirudisha kwangu.

Uvulini mwa mauti,
Siachi hatari kamwe,
Wewe Bwana huniachi,
Mwokozi wangu wewe.

Waniandikia meza
Neema kwako tele.
Kwa wewe, yote naweza.
Na msalaba mbele.

Kamwe hautapungua
Uule wema wako;
Mwisho, atanichukua,
Juu, niimbe kwako.

115.Kilima kando Ya Mji


Kilima kando ya mji
Alikufa Bwana;
Kuokoa wakosaji
Akateswa sana.

Kabisa hayasemeki,
Mateso dhaifu
Alikufa mwenye Haki
Tupate wokovu.

Alimwaga damu yake
Ili tuwe wema,
Tufae kukaa kwake
Mbinguni daima.

Hatuna mwenye imani
Aliye na haki,
Wa kutosha yetu deni,
Rafiki Yesu tu.

Alijua peke yake
Kufungu Mbingu
Ufunguo damu yake
Kondoo wa Mungu.

Aliyetupenda hivyo
Nasi tumpende,
Tukamtumai vivyo
Na kazi tutende.

114.Bwana Mungu, Nashangaa Kabisa


Bwana Mungu, nashangaa kabisa
Nikitazama kama vilivyo
Nyota, ngurumo, vitu vingi vyote
viumbwavyo kwa uwezo wako.

Roho yangu na ikuimbie
Jinsi Wewe ulivyo Mkuu,
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi Wewe ulivyo Mkuu.

Nikitembea pote duniani,
Ndege huimba, nawasikia,
Milima hupendeza macho sana,
Upepo nao nafurahia.

Nikikumbuka kama Wewe Mungu
Ulivyompeleka Mwanao,
Afe azichukue dhambi zetu,
Kuyatambua ni vigumu mno.

Yesu Mwokozi utakaporudi
Kunichukua kwenda Mbinguni,
Nitashukuru na kwimba milele,
Wote wajue jinsi ulivyo.

117.Tufani Inapovuma


Tufani inapovuma
Sana moyoni mwangu,
Huona pa kujificha
Mkononi mwa Mungu.

Hunificha, hunificha
Adui hatanipata,
Hunificha, hunificha,
Mkononi mwake.

Pengine kuna taabu
Yanisongeza kwake;
Naijua si hasira,
Ni ya mapenzi yake.

Adui wakiniudhi
Nami nikisumbuka,
Mungu atavigeuza
Vyote viwe baraka.

Niishipo duniani
Ni tufani daima,
Anilindapo rohoni
Nitakaa salama.

116.Bwana U Sehemu Yangu


Bwana u sehemu yangu, rafiki yangu wewe;
Katika safari yangu, tatembea na wewe;
Pamoja na wewe, pamoja na wewe,
katika safari yangu, tatembea na wewe.

Mali hapa sikutaka, ili niheshimiwe,
na yanikute mashaka, sawa sawa na wewe.
Pamoja na wewe, pamoja na wewe,
heri nikute mashaka sawasawa na wewe.

Niongoze safarini, mbele unichukue,
mlangoni kwa mbinguni, niingie na wewe.
Pamoja na wewe, pamoja na wewe,
mlangoni kwa mbinguni, niingie na wewe.

119.Si Damu Ya Nyama


Si damu ya nyama
Iliyomwagika
Iwezayo kuondoa
Dhambi za wakosa.

Yeye Bwana Yesu
Sadaka ya Mungu,
Mwenye damu ya thamani,
Ni mwokozi kweli.

Kwa imani yangu,
Namshika yeye,
Naziweka dhambi zangu
Juu ya kichwa chake.

Mzigo wa dhambi
Sichukui tena,
Ameuchukua yeye,
Juu ya msalaba.

Bwana Yesu ndiye,
Mwokozi wa kweli
Tumsifu siku zote,
Twapata uhuru.

118.Ni Ujumbe Wa Bwana


Ni ujumbe wa Bwana, Aleluya!
wa maisha ya daima,
Amenena mwenyewe, Aleluya!
Utaishi ukitazama.

Tazama, ishi sasa!
Kumtazama Yesu,
Amenena mwenyewe, Aleluya!
Utaishi ukitazama.

Ni ujumbe wa wema, Aleluya!
Nawe shika, rafiki yangu!
Ni habari ya raha Aleluya!
Mwenye kuinena ni Mungu.

Uzima wa daima,Aleluya !
Kwake Yesu utauona.
ukimtazama tu, Aleluya!
Wokovu u pweke kwa Bwana.

Monday, December 5, 2016

120.Enyi Wanadamu

Enyi wanadamu mbona
Sana mwatanga-tanga,
Kama kondoo wanyonge,
Wasio na mchunga?
Yuko mchunga mmoja
Mwenye mapenzi mema;
Haya kutaneni kwake,
Atawachunga vyema.

Mungu tunamwona kuwa
Mwenye uwezo wote;
Na nguvu zake zapita
Mawazo yetu yote:
Ni Baba,mapenzi yake
Ni makubwa hakika;
Hatuwezi kuyajua,
Na hayana mpaka.

Rehema za Mungu nazo
Zina upana sana;
Kama huo wa bahari,
Mwisho wake hapana;
Haki yake ina mema,
Kwa hayo twashukuru,
Kwetu uko msamaha,
Furaha na uhuru.

Mapenzi yake mapana,
Sisi hatuna cheo
Cha kutosha, nao moyo
Una wema upeo;
Ukombozi mwingi mno
Katika damu yake;
Sote twapata furaha,
Kwa maumivu yake.

Yesu mkaribieni
Njoni msife myoyo;
Njoni kwake kwa imani,
Mema yake ni hayo;
Heri tuwe kama wana
Tushike neno lake,
Daima atujaza
Tele furaha yake.

121.Liko Lango Moja Wazi

Liko lango moja wazi,
Ni lango la mbinguni;
Na wote waingiao
Watapata nafasi.

Lango ndiye Yesu Bwana
Wote waingie kwake,
Lango! Lango
La Mbinguni ni wazi.

Yesu ndiye lango hili,
Hata sasa ni wazi,
Kwa wakubwa na wadogo,
Tajiri na maskini.

Hili ni lango la raha,
Ni lango la rehema;
Kila mtu apitaye
Hana majonzi tena.

Tukipita lango hili
Tutatua mizigo,
Tuliochukua kwanza,
Tutavikwa uzima.

Hima ndugu tuingie
Lango halijafungwa,
Likifungwa mara moja
Halitafunguliwa.

122.Bwana Yesu

Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mbona unaumia? Unateseka sana,
Kwa ajili ya kuomba,
Waomba na jasho jingi likageuka damu.

Kumbe! Ni dhambi zangu zinazokuumiza.
Bwana wangu, Mungu wangu,
Mimi leo, naja kwako
Ili niziungame.

Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mbona unaumia, na mizigo mizito?
Umejitwalia wewe, msalaba mabegani
Kwa ajili ya watu.

Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mbona unatukanwa, wawambwa kama mwizi,
Bila kosa ukalia, Baba yangu, wasamehe,
Chukua roho yangu.

Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Muda ulipofika, nchi ikawa giza,
Mbinguni pakatulia,
Angani pakawa kimya,
Watu wakaogopa.

Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Jinsi ulivyoumwa, ukamwomba Baba,
Leo umeshinda kifo, sasa wapaa Mbinguni,
Naimba, Haleluya.

123.Nimeketi Mimi Nili Kipofu

Nimeketi mimi nili kipofu
Gizani nangojea macho;
Ewe Bwana Yesu mwenye wokovu,
Ondoa dhambi zangu nzito.

Huruma hakuna aonaye,
Gizani nagojea macho,
Sasa nitakase nikusihiye,
Yesu, na dhambi zangu nzito.

Tangu siku nyingi nimepofuka
Natamani uso nikwone;
Ewe Bwana Yesu, mwenye baraka
Sema neno, basi, nipone.

Nimeketi mimi nili na giza,
Nami ya kutumai sina;
Ili nasikia kunong’oneza,
“Kwake Yesu kuna kupona.”

Sunday, December 4, 2016

124.Mungu Ulisema

Mungu ulisema,
Giza ilikoma;
Twakushukuru!
Twakusihi sote,
Duniani mote
Na kwa watu wote,
Iwe nuru.

Yesu ulikuja,
Ulituletea
Nuru kuu;
Macho kwa vipofu,
Maisha kwa wafu;
Twakushukuru.

Roho kiongozi,
Roho wa mapenzi
Tia nuru;
Mwovu hata sasa
Watu huwatosa,
Tunakwomba hasa,
Iwe nuru.

Mungu wa utatu
Mwanga wao watu,
Tuwe huru;
Twende kote-kote
Wafundishwe wote,
Duniani mote,
Iwe nuru.

125.Ati Twonane Mtoni?

Ati twonane mtoni?
Maji mazuri ya Mbingu;
Yanatokea mwangani,
Penye kiti cha Mungu.

Naam, twonane mtoni!
Watakatifu, kwenu ni mtoni!
Tutakutanika mtoni
Penye kiti cha Mungu.

Tukitembea mtoni
Na Yesu mchunga wetu
Daima tu ibadani
Usoni pake kwetu.

Kwang’ara sana mtoni
Cha Mwokozi ni kioo,
Milele hatuachani,
Tumsifu kwa nyimbo.

Si mbali sana mtoni,
Karibu tutawasili,
Mara huwa furahani
Na amani ya kweli.

126.Ni Mji Mzuri

Ni mji mzuri,
Mbali sana;
Watu wanawiri
Kama jua;
Waimba kwa tamu,
Tuna wema hakimu:
Sifa na idumu,
Kwake Bwana.

Ni mji mzuri
Twende sote!
Una na fahari
Msikawe!
Raha tutaona,
Dhambi hapana tena;
Hatutaachana
Siku zote.

Ni mji mzuri;
Macho yote
Huko wanawiri
Kama pete;
Baba tutamwona,
Tukifanywa tu wana;
Tumo kupendana
Naye sote.

Ni mji mzuri;
Tusipotee
Na tuwe hodari,
Tuupate!
Tufunze, tutume
Kwa taji na ufalme:
Sifa na zivume
Siku zote.

127.Bwana Yesu Atakuja

Bwana Yesu atakuja, Vumilia!

Omba, ukiwa na haja, Vumilia!

Mbingunu Mungu aliko, Mwamini Mwokozi wako,

Nawe utafika huko, Vumilia!

Ikikucheka dunia, Vumilia!

Mwovu atakuvizia, Vumilia!

Hataweza kukushinda, Bwana Yesu akulinda,

Roho yako, akupenda, Vumilia!

Na ukiwa hatarini, Vumilia!

Dhiki nyingi duniani, Vumilia!

Vyatupasa kuyakuta, Majaribu na matata,

Na Bwana hakutuficha; Vumilia!

Adui wakikutana, Vumilia!

Na ndugu wakikukana, Vumilia!

Zote, zote zitakwisha, Nguvu zote za kutisha

Mungu chini atashusha; Vumilia!

Moyoni una majonzi, Vumilia!

Ndiyo bonde-ya-machozi, Vumilia!

Hima tutaandamana, Kwetu Mbinguni na Bwana

Tena hatutaachana; Vumilia!

128.Mmoja Apite Wote

Mmoja apita wote,
Atupenda;
Zaidi ya ndugu wote,
Atupenda;
Rafiki wa duniani,
Wote hatuwaamini;
Yesu kwa kila zamani,

Atupenda.
Kumjua ni uzima,
Atupenda;
Jinsi ajaavyo wema
Atupenda;
Yeye ametununua
Kwa damu aliyomwaga,
Dhambini kutuokoa,
Atupenda.

Sasa tunaye rafiki,
Atupenda;
Hupenda kutubariki;
Atupenda;
Twapenda kumsikia,
Atwita kukaribia,
Nasi tutamwamania,
Atupenda.

Husamehe Dhambi zetu,
Atupenda;
Hushinda adui zetu,
Atupenda;
Anatwonea huruma,
Hatupati ila mema,
Anatwongoza salama,
Atupenda.

129.Karibu Na Wewe

Karibu na wewe,
Mungu wangu
Karibu zaidi,
Bwana wangu
Siku zote niwe
Karibu na wewe,
Karibu zaidi
Mungu wangu.

Mimi nasafiri
Duniani,
Pa kupumzika
Sipaoni,
Nilalapo niwe
Karibu na wewe,
Karibu zaidi
Mungu wangu.

Na kwa nguvu zangu
Nikusifu;
Mwamba, uwe maji
Ya wokovu;
Mashakani niwe
Karibu na wewe;
Karibu zaidi
Mungu wangu.

Na nyumbani mwa juu,
Baba yangu,
Zikikoma hapa
Siku zangu,
Kwa furaha niwe
Pamoja na wewe,
Karibu kabisa
Mungu wangu.

130.Niongoze,Bwana Mungu

Niongoze, Bwana Mungu,
Ni msafiri chini;
Ni mnyonge, nguvu sina:
Nishike mkononi;
U mkate wa Mbinguni,
nilishe siku zote.

Kijito cha maji mema,
Kitokacho mwambani,
Nguzo yako, moto, wingu,
Yaongoza jangwani;
Niokoe mwenye nguvu;
Nguvu zangu na ngao.

Nikikaribia kufa,
Sichi neno lolote,
Wewe kifo umeshinda
Zinawe nguvu zote,
Tutaimba sifa zako,
Kwako juu milele.

131.Piga Sana Vitu Vyema

Piga sana vita vyema
Kwa ushujaa daima,
Yesu ndiye nguvu zako,
Yesu ndiye kweli yako.

Kaza mwendo, ushindane
Angaza macho, umwone
Yesu ndiye njia yako,
Naye ndiye tuzo lako.

Tupa kizito, simama,
Tazama mbele, si nyuma;
Ni yeye uzima wako,
Naye ni kipendo chako.

Tangamka, uamini
Akushika mikononi
Hageuki, akupenda,
Kuwa naye una pia.

132.Sauti Sikilizeni

Sauti sikilizeni
Za waimbao juu,
“Aleluya, Aleluya,
Aleluya, mkuu!”
Wako makundi-makundi
Kama nyota wang’ara,
Kwa makuti ya mitende,
Na meupe wamevaa.

Wazazi na manabii
Wafanyaji wa njia;
Mashahidi, waandishi,
Nao wafalme pia!
Mabikira kina-mama,
Wajane wa kusali,
Waimba wakikutana
“Msifunu Imanweli”.

Watu toka huzunini
Wameosha na nguo,
Ni kwa damu yake Yesu;
Maonjo, mbali nao!
Walitekwa, walikatwa
Hata kwa misumeno,
Kwao kifo na shetani
Walishindiwa mno.

Mungu mumo mwake Mungu,
Nuru mumu mwa nuru,
Kwa kufungamana mwako
Tutaishi mahuru;
Tujalize, Imanweli,
Kujaa kwako wewe
Mungu Baba, Mungu Mwana,
Mungu Roho, tunawe.

133.Ni Wako Mungu!

Ni wako Mungu!
Ni furaha kwangu,
Ni raha kumjua mwokozi wangu.

Aleluya enzi ndako;
Aleluya,Amin.
Aleluya,enzi ndako;
Rejea Yesu.

Mwana wa Mungu
Ndiye fungu langu,
Na moyo hufurahi kwa Yesu wangu.

Raha ya kweli
Ina jina hili,
Na aliyeshika,ana Mbingu kweli.

Nimeingia
Mapendano haya,
Nimepata uzima na Mbingu pia.

Nilipo chini,
Ni mwako kazini
Hata nije kwako uliko Mbinguni.

134.Juu Yake Langu Shaka

Juu yake langu shaka,
Yesu namuwekea,
Nami sitafedheheka
Nikimtegemea.

Natumai, natumai,
Nnatumai kwake tu;
Natumai, natumai,
Natumai kwake tu.

Juu yake, dhambi zangu;
Aniosha kwa damu;
Nionekane kwa Mungu,
Nisiye na laumu.

Juu yake yangu hofu;
Kwake nimetulia;
Sipotei kwa upofu
Njia aning’azia.

Juu yake raha yangu;
Humuangalia tu;
Mwenye kila ulimwengu,
Aniruzuku na huu.

Juu yake, moyo wangu;
Hali yangu na mali;
Mimi wake, Yeye wangu,
Twapasana kamili.

135. Mapenzi Ya Milele

Mapenzi ya milele
Ndiyo yanipendezayo;
Yalinipenda mbele,
Sina fahamu nayo;
Sasa amani yake
Tele rohoni mwangu,
Ni mimi kwa kuwa wake,
Na yeye kuwa wangu,
Ni mimi kuwa wake,
Na yeye kuwa wangu

Mbingu zinang’ara juu,
Na nchi nayo vivyo;
Macho ya dunia tu
Hayajaona hivyo;
Nyuni huimba sana,
Maua yana rangi,
Ni kumjua Bwana
Na pendo zake nyingi,
Ni kumjua Bwana
Na pendo zake nyingi,

Mambo mengi maovu
Nayo yenye kutisha,
Sasa hayana nguvu,
Si yenye kututisha;
Ni mkononi mwake,
Nalindwa salamani
Ninajua ni wake,
Ni wake mapenzini.
Ninajua ni wake,
Ni wake mapenzini.

Wake hata milele,
Si kutengana tena;
Hunipa raha tele
Moyoni mwangu, Bwana;
Hiyo nchi na Mbingu
Zitatoweka zile,
Ni wake, Yeye wangu,
Milele na milele.
Ni wake, Yeye wangu,
Milele na milele.

136.Msifuni, Yesu Ndie Mkombozi

Msifuni ,Yesu ndiye mkombozi;
Imbeni ya pendo zake kuu,
Sujuduni,malaika mlioko,
Jina lake liwe na sifa kuu.
Kama vile mchunga uchungavyo
Vivyo sisi kutwa atachunga.
Msifuni mlio wakw watoto
Msifuni aliye mchunga.

Msifuni,Yesu ndiye mkombozi;
Akateswa tupate ongoka;
Ndiye Mwamba,Dhamana ya kuokoka;
Sujuduni kwake muangikwa,
Yesu aliyeudhiwa na hamu
Kwa pendo za baba yake Mungu.
Aliyefyolewa na kusulubiwa.
Msifuni ndilo letu fungu.

Msifuni,Yesu ndiye Mkombozi;
Shindukeni,enyi malango juu;
Bwana Yesu tangu milele Mwokozi,
Mvikeni taji, ni yake tu.
Atakuja kuitawala nchi,
Yesu,Mwombezi wetu wa Mungu.
Msifuni, ni mfalme wa salama;
Ndiye kweli mwana wake Mungu.

137.Yesu Mponya

Yesu ndiye mganga wetu
Aponya wagonjwa wote;
Mganga wetu ni Yesu,
Aponyaye hasira.

Tumsifu huyo Yesu
Tumsifu milele,
Kwani Mponya mtakata
Mwokozi wa wanyonge

Mganga wetu ni Yesu
Huondoa matusi;
Mganga wetu ni Yesu,
Mwenye kuponya choyo.

Mganga wetu ni Yesu
Huponya wivu wetu;
Yesu ndiye aponyae
Kelele za nyumbani.

Mganga wetu ni Yesu
Mponya wa tamaa mbaya;
Mganga wetu ni Yesu
Uasherati hufuta

Mganga wetu ni Yesu
Aponya kiu cha pombe,
Mganga wetu ni Yesu
Kila dhambi uponya

138.Tukutendeleza ( Luganda )

Yesu, Mulokozi wange:
Lero nze wuwo wenka;
Omusaigwo gunazi’za
Yesu Mwana gwendiga.

Tukutendereza, Yesu,
Yesu Mwana gwendiga;
Omusaigwo gunazi’za;
Nkwebaza, Mulokozi.

Eda nafuba bufubi
Okufuna, emirembe;
Lero maliride dala
Okweyabiza Yesu.

Nababuliranga bantu
Obulokozi bwona,
Obutali bwa kitundu
Obulamba obwobuwa

Nategezanga ebya Yesu
Nobuvumunesitya;
Eyanziya mu busibe
Nokuwonya eyamponya.

Nebaza eyanunula nze;
Eyamponya wa kisa!
Yesu ankuma
Ansanyusaera,
Bulijo yebazibwe.